HATIMAYE MBOWE AWASILISHA USHAHIDI POLISI KUHUSU MLIPUAJI WA BOMU ARUSHA
HATIMAYE Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), Freeman Mbowe, jana amewasilisha kwa maandishi ushahidi wake
makao makuu
ya Jeshi la Polisi mjini Dar es Salaam. Maelezo ya Mbowe ambayo jana
yaliwasilishwa, yamekuwa siri nzito, kwani yanatokana na msimamo wa
CHADEMA kudai wana ushahidi na tukio la mauaji ya mlipuko wa bomu
lililotokea Juni 15, mwaka huu mkoani Arusha.
Wakili wa Mbowe, Peter Kibatala alilithibitishia MTANZANIA
mjini Dar
es Salaam jana, kuwa aliwasilisha saa 5 asubuhi ambapo alipokelewa na
Mkuu wa Idara ya Operesheni za Upelelezi Tanzania (CID), Kamishna
Advocate Nyombi.
Baada ya kuwasilisha maelezo hayo, Wakili
Kibatala alikataa katakata kuzungumzia kilichomo ndani ya maandishi
hayo, kwa madai kuwa ni siri yao na polisi.
“Nathibitisha bila
shaka, nimewasilisha majibu kwa niaba ya Mbowe leo (jana), makao makuu
ya polisi kama tulivyokubaliana, lakini yaliyoandikwa humo ni
siri…siwezi kuzijadili tusubiri kutoka kwao,” alisema Kibatala.
Hatua ya kuwasilisha majibu hayo kimaandishi, ilifikiwa Jumatano wiki hii katika mahojiano baina ya Polisi na Mbowe.
Siku
hiyo,
Mbowe aligoma kuwasilisha ushahidi wake polisi kama alivyotakiwa kwenye
barua aliyoandikiwa na jeshi hilo Julai 17, mwaka huu, kwa kile
alichosema hadi Rais Jakaya Kikwete atakapounda tume ya kijaji
kuchunguza tukio hilo.
Katika barua hiyo, Mbowe alitakiwa kufika bila kukosa akiwa na ushahidi wa mauaji ya mlipuko wa bomu hilo.
Hata
hivyo,
Mbowe aliripoti kuitikia wito wa barua hiyo, lakini aliendelea
kushikilia msimamo wake wa kutowasilisha ushahidi huo kwa polisi.
Jeshi
la
Polisi, limekuwa katika mvutano na Mbowe likimtaka kuwasilisha ushahidi
kuhusu mlipuko wa bomu hilo, katika Uwanja wa Soweto wakati wa mkutano
wa kuhitimisha kampeni za uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata
nne na kuua watu wanne na kujeruhi wengine 70, katika uwanja huo
ushahidi ambao alidai anao.
Endapo Mbowe atakutwa na hatia ya kutokuwa na ushahidi huo, atakumbwa na adhabu ya miaka mitatu jela au faini ya Sh 500,000.
Hii
ni
kwa mujibu wa Jeshi la Polisi katika barua yake kwa Mbowe, ikunukuu
kifungu cha sheria ya kifungu cha 10(2) na (2A) cha sheria ya mwenendo
wa makosa ya jinai nchini, sura ya 20, kama ilivyorekebishwa mwaka 2002.
No comments:
Post a Comment