facebook likes

Monday, July 29, 2013

BAYERN MUNICH YAIPA CHELSEA PAUNI MILIONI 40 KWA AJILI YA DAVID LUIZ, MOURINHO SASA...

KLABU ya Bayern Munich imepanga kufufua mpango wa kumsajili David Luiz na imeandaa dau la Pauni Milioni 40 kuhakikisha inamnasa.
Kocha wa Bayern, Pep Guardiola anaona beki huyo wa kati atasaidia sana kuimarisha ukuta wa mabingwa hao wa Ulaya na kwa muda mrefu amekuwa akimzimikia Luiz.
Chelsea ilimtuliza beki huyo Mbrazil mwenye umri wa miaka 26, kwa kumsainisha Mkataba mpya wa miaka mitano Septemba mwaka jana, na imesema hauzwi na kocha Jose Mourinho alijaribu kupuuza maoni kwamba Luiz si aina ya beki wa kati wakati wa ziara ya timu hiyo Asia.
Wanted: Bayern Munich are ready to make a £40million-plus offer for Chelsea defender David Luiz
Anatakiwa: Bayern Munich iko tayari kutoa Pauni Milioni 40 au zaidi kwa ajili ya beki wa Chelsea, David Luiz
No issue: Chelsea boss Jose Mourinho has refuted claims Luis is not his sort of player as a defender
Hakuna mpango: Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho amekanusha madai kwamba Luis hafai kuwa beki wa kati kwake
Instructing: Bayern manager Pep Guardiola has identified the defence as an area to be improved upon
Maelekezo: Kocha wa Bayern, Pep Guardiola anataka kuimarisdha safu yake ya ulinzi

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...