Mheshimiwa Peter Msigwa akifunguka katika kipindi cha Makutano na Fina Mango
Fina Mango akimsikiliza Mchungaji Peter Msigwa wakati akijibu moja ya maswali katika kipindi cha Makutano.
Mbunge
wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa amesema Tanzania sio mali ya
chama chochote cha siasa wala kundi lolote la watu wakati akihojiwa
katika kipindi cha Makutano na Fina Mango.
Mheshimiwa Peter
Msigwa alitoa kauli hiyo alipoulizwa anaonaje mwamko wa kufanya
mabadiliko unaoendelea ikiwemo mchakato wa katiba mpya.
Aliwalaumu
watu wa kipato cha kati kwa kusema wao ndio kikwazo cha maendeleo kwa
sababu ya kuridhika na vitu vidogo walivyovipata, "Kila mtu aingie
acheze huu mchezo kwamba ni wakati uliofika wa kuibadilisha Tanzania,
tuibadilishe kifikra.
Watu wengi mmekaa maofisini na kompyuta
zenu na vijumba vidogo mmejenga na vigari vidogo mmeweka nje mnaogopa,
lakini kama tutaendelea kuruhusu akili ndogo iendelee kutawala
hatutaenda popote" alisema Mheshimiwa Msigwa.
Hata hivyo
aliipongeza tume ya katiba kwa kusema ameridhishwa na ilivyofanya kazi
yake kutokana na hofu waliyokuwa nayo baada ya mchakato wa kuandaa
katbiba mpya ambao ulianzishwa na CHADEMA kuchukukuliwa na kugeuzwa
agenda ya chama tawala na hivyo kuleta wasiwasi wa haki isingetendeka
hasa ile ya uwakilishi katika utoaji maoni ya katiba.
No comments:
Post a Comment