facebook likes

Monday, July 29, 2013

MAN CITY YAENDELEA KUTAKATA, PELLEGRINI ATWAA TAJI LA KWANZA BAADA YA KUWAFUMUA SUNDERLAND 1-0 HONG KONG


BAO pekee la Edin Dzeko limeipa ushindi Manchester City dhidi ya Sundeland katika michuano ya Barclays Asia Trophy , huo ukiwa ushindi wa pili kwa kocha Manuel Pellegrini Hong Kong baada ya kufungwa mechi zote mbili Afrika Kusini.
Kikosi cha Pellegrini kimefanikiwa kumaliza juu ya wapinzani wao wa England, Sunderland na Tottenham na kutwaa Kombe la michuano hiyo ya timu za Ligi Kuu.
Kikosi cha Manchester City kilikuwa: Pantilimon; Zabaleta, Kompany, Nastasic/Lescott dk75, Clichy/Kolarov dk62, Milner/Navas dk46, Toure/Fernandinho dk62, Garcia, Silva/Nasri dk46, Dzeko na Negredo/Barry dk79.
Sunderland: Mannone; Gardner, O’Shea, Brown, Colback; Johnson/Karlsson dk61, Larsson, Cabral/Ba dk46, Giaccherini/McClean dk76, Altidore/Wickham dk46 na Sessegnon/Mandron dk88.
Juu kuchukua Kombe: Vincent Kompany akiinua Kombe la Barclays Asia 

Edin kikosi cha kwanza: Edin Dzeko wa Man City alifunga bao pekee la ushindi

Mechi yao leo ilichezwa kwenye mvua na makipa walikuwa wana kibarua kizito cha kudaka, kwani mipira ilikuwa inateleza mikonon


No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...