facebook likes

Monday, July 29, 2013

UKIMWI WAMTESA MSANII BABY MADAHA,ATOA TAMKO ZITO NA LA KUSHANGAZA. MCHUNGAJI AMPA USHAURI WA BURE KUNUSURU MAISHA YAKE!

Msanii wa Bongo muvie na muziki Baby Madaha.
 
Msanii  wa  filamu  bongo,Baby Madaha  amefunguka  kwamba  siku  akianza  kuona  dalili  za  ugonjwa  wa  UKIMWI  ndani  ya  mwili  wake   atakunywa  sumu  kwa  kuhofia  kuchekwa  na  jamii.
Akiongea  na  mwandishi  wetu,Madaha  amedai  kuwa  kwa  sasa  anaamini  hana  ngoma  maana  siku  zote  hutumia  Kinga (kondom)   ili  asiambikizwe  gonjwa  hilo  japo  hana  uhakika  asilimia  zote  maana  hiyo  ni  mipango  ya  mungu.

"Siukatai  ugonjwa  huo  kwa  kuwa  sijui  ni  lini  naweza  kuupata  hasa  ukizingatia  kwamba  mimi  bado  ni  kijana  mbichi  ambaye  bado  nahitaji  kuifurahia  dunia"...Alisema  Baby Madaha..
Katika  mazungumzo  hayo, Madaha  anadai  kwamba  mpaka  sasa  hakuna  mpenzi  wake  yeyote  aliyekufa  kwa  Ngoma  ingawa  wapo  waliofariki  kwa  maradhi  ya  kawaida  na  ajali....
"Nikijua  tu  nina  ngoma  ni  lazima  ninywe  sumu  ili  kukwepa  balaa  la  wabongo.Najitahidi  kujilinda  ili  nisiudake  mapema"..Alisema Madaha 
Madaha  anadai  kwamba  kitendo  cha  yeye  kujiua  mapema  kitasaidia  kuwaondolea  wasiwasi  wasanii  wenzake  ambao  wataanza  kujiuliza  maswali  mengi  kuhusu  watu  aliowahi  kutoka  nao  kimapenzi
"Nitawasaidia  wasanii  wengine  ambao  nimewahi  changia  nao  mabwana.Najua  wataumia  sana, lakini  ndo  hivyo  tena, hakutakuwa  na  jinsi."Sijasema  nina  UKIMWI,Hapana,nimesema  kwamba  ikitokea  maana  watu  hawakawii  kupindisha  maneno"..Madaha
 
Hata hivyo mchungaji wa Kanisa la kiroho aliyejitambulisha kwa jina la Jemsi Mgundoi amempa ushauri wa bure msanii huyo na kusema" Nimesoma taarifa ya msanii huyo ya kuwa akigundulika ameathirika na UKIMWI atajiua, asifanye hivyo kwani atakuwa amejiongezea dhambi mbele za Mungu wake aliyehai hivyo anachotakiwa kufanya ni kuacha zianaa tu na si vinginevyo" Alisema mtumishi huyo wa bwana

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...