MCHEZAJI wa zamani wa
kimataifa wa Ujerumani, Oliver Bierhoff anaamini kuwa uchache wa
wachezaji katika vilabu vya Bayern Munich na Borussia Dortmund ambao
wanacheza katika timu ya taifa ya nchi hiyo unaweza kuwanyima nafasi ya
kufanya vizuri katika michuano ya Kombe la Dunia mwakani. Pamoja
na mafanikio makubwa ambayo timu hizo mbili imeyapata katika michuano
ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya msimu uliopita, Bierhoff ameonyesha
wasiwasi wake kwa mwenendo wa timu ya taifa. Badala
yake nguli huyo mwenye miaka 45 ametaka hatua za makusudi kwa vilabu
vikubwa kuthamini vipaji vya vijana ili kuokoa soka la nchi hiyo lisije
kuporomoka. Bierhoff
amesema pamoja na Ujerumani kujivunia wachezaji nyota kama Mario Gotze,
Mesut Ozil, Thomas Muller na Toni Kroos lakini nchi hiyo bado
inakabiliwa na changamoto ya kukosa washambuliaji pamoja na mabeki wa
daraja la juu. Nguli huyo amesema kwasasa wanatakiwa kujipanga ili kuhakikisha wanaziba mapengo yaliyopo na kuendelea kubakia katika ushindani.
No comments:
Post a Comment