KLABU ya Al Ahly ya
Misri imeliomba Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF kusogeza mbele
mchezo wao dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini mpaka Agosti 9
mwaka huu. Mkurugenzi
wa michezo wa Al Ahly Sayed Abdul Hafez alithibitisha timu hiyo
kuandika barua rasmi kwa CAF ya kusogeza mbele mchezo huo mpaka Agosti 9
badala ya Agosti kama ulivyopangwa kwasababu ya mfungo wa mwezi wa
Ranadhan ambapo wacheza wengi wa timu hiyo wanakuwa wamefunga. Hafez
pia aliongeza kuwa Wizara ya mambo ya Ndani ya nchi hiyo imekataa
kuwawekea ulinzi kwa ajili ya mchezo huo jijini Cairo au Alexandria
hivyo wanatarajia mechi hiyo kuchezwa katika mji wa El Gouna au Aswan. Hafez
amesema wamefikia hatua hiyo baada ya timu hiyo kucheza dhidi ya
Zamalek mchana na wachezaji kukataa kufungulia ambapo wote waliathirika
mpaka hivi sasa kutokana na kucheza kwenye jua kali huku wakiwa
wamefunga. Naye
kocha wa Pirates Roger De Sa ameonyesha wasiwasi wake wa kucheza na Al
Ahly jijini Cairo kutokana na vurugu zinazoendelea lakini anaamini kuwa
CAF itatoa uamuzi sahihi kuhusiana na mahali patakapochezwa mchezo huo.
No comments:
Post a Comment