SEMENYA ASHINDWA KUFUZU MASHINDANO YA DUNIA.
MWANARIADHA nyota wa
kike kutoka Afrika Kusini, Caster Semenya atashindwa kushiriki
mashindano ya riadha ya dunia mwezi ujao baada ya kushindwa kufuzu
katika mbio za mchujo zilizofanyika nchini Ubelgiji. Semenya
alifanikiwa kushinda mbio za mita 800 katika mashindano hayo ya mchujo
yaliyofanyika jijini Nivone kwa kutumia muda wa dakika 2 sekunde 01.86
lakini muda huo haukutosha kumfanya kufikia kiwango kilichohitajika
ambacho ni dakika 2 sekunde 01.50. Katika mbio hizo Sanne Verstegen wa Uholanzi alimaliza katika nafasi ya pili akitumia muda wa dakika 2 sekunde 02.09. Hiyo
ni mara ya kwanza kwa Semenya kushindana toka katika michuano ya
olimpiki iliyofanyika jijini London mwaka jana baada ya kipindi kirefu
kukaa kando kutokana na maumivu ya goti.
No comments:
Post a Comment