(picha kwa hisani ya ITV)
Waziri wa uchukuzi Dk. Harison Mwakyembe amefanya ziara ya kushtukiza kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar-es-Salaam
..SOMA ZAIDI...
na kubaini kuwa upitishwaji wa madawa ya kulevya uwanjani hapo hufanywa kwa msaada wa baadhi ya wafanyakazi wanaoshirikiana na wasafirishaji hao kupitisha shehena hizo.
Waziri Mwakyembe aliwasili uwanjani hapo majira ya
saa kumi na mbili alfajili na kutaka kuonyeshwa hatua ya mwanzo hadi
mwisho ya ukaguzi wa mizigo uwanjani hapo na kupokea taarifa toka kwa
mamlaka zinazosimamia uwanja huo.
Naye mkurugenzi wa uwanja huo Bw Moses Malaki
amesema uwanja unakidhia matakwa ya kiusalama wa kimataifa ila jambo
kubwa ni uwepo wa watau wachachae ambo wanafanya kazi kinyume na mfumo
huo.
Akihitimisha ziara hiyo Mh Mwakyembe amesema
amebaini mambo mengi ikiwemo kuwa katika uwanja huo kuna taasisi nyingi
za kiusalama ambazo zinafanya kazi hivyo na kusema kuwa hakuna sababu
yeye wala watumishi wengine wa uwanjani huo kuendelea kufanya kazi
uwanjani hapo.
Hivi karibuni uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wa jijini Dar-es-Salaam, uligubikwa na
wingu la kukamatwa kwa kiasi kikubwa cha madawa ya kulevya yaliyo
kamatwa nchini Afrika ya kusini yakihusishwa na vijana kutoka Tanzania,
jambo lililopelekea Watanzania kukaguliwa ki ziada katika mataifa ya nje
ikiwemo Afrika ya kusini hivyo kuchafua jina la Tanzania katika medani
ya kimataifa
Chanzo:ITV
No comments:
Post a Comment