Taarifa hizo za kijeshi zemesema kuwa
kiongozi huyo aliyeuwawa ni Momodu Bama,ambaye ni wa pili katika uongozi
wa kundi hilo la wapiganaji.
Mapema mwezi huu wafuasi wengine wa kundi
hilo la Boko Haram ambao walikuwa wamekamatwa walifichua kwamba huyo
kamanda wao alikuwa ameuawawa.
Msemaji wa Jeshi Brig Jenerali Chris
Olukolade amesema Momodu Bama, ambaye pia anafahamika kama "Abu Saad",
alikuwa na ujuzi wa kufyatua makombora ya kutungua ndege.
Mapema mwezi wa Mei, Nigeria ilitangaza
hali ya hatari katika maeneo ya kaskazini Mashariki mwa nchi ili
kupambana na wapiganaji wa Boko Haram.
Hata hivyo hadi sasa hakuna taarifa huru
kuthibitisha kuuwawa kwa Bwana Momodu Bama nao Boko Haram wenyewe hawaja
thibitisha kifo cha kiongozi huyo.
Jenerali Olukolade, alisema Momodu Bama
alikuwa ni mmoja ya viongozi wa Boko Haram waliokuwa wakitafutwa zaidi
na kulikuwa kuna zawadi ya dola $155,000, £100,000 kwa yeyote atakaye
toa habari zitakazosaidia kukamatwa au kuuwawa kwake
No comments:
Post a Comment