
Msanii nyota kwenye tasinia ya muziki
 na filamu bongo Zuwena Mohamed “ Shilole” mwishoni mwa wiki iliyopita 
alionja joto ya jiwe baada ya kutiwa mtu kati na wakina dada waliokuwa 
wanamdai kiasi kikubwa cha pesa.
Habari za uhakika zilizothibitishwa 
na mmoja wa wakina dada hao waliokuwa wanamdai zilisema kuwa wanawake 
hao waliamua kuchukua hatua za kumtia adabu Shilole baada ya kupata 
taarifa kuwa siku hiyo alikuwa ana hama kwa kukimbia na teni lao “ Ishu 
ilikuwa hivi sisi tunamdai huyu dada lakini cha kushangaza amekuwa 
akitupiga chenga sana na ona alivyokuwa sio mstaarabu kumbe siku hiyo 
alikuwa anahama na deni letu ndio maana tuliamua kwenda kumzingua” 
Alisema dada huyo aliomba jina lake lihifadhiwe.
Dada huyo aliendelea kufunguka mengi 
kuhusu sakata hilo “ Unajua sisi tunafanya biashara zetu hivyo kuna siku
 Shillole alikuja na kusema amekwama kipesa hivyo tumuazime pesa na 
tukafanya hivyo lakini cha kushangaza mwezi wa sita huu hataki kurudisha
 na amekuwa akitukwepa mara kwa mara hivyo majirani ndio wakatushtua 
kuwa anataka kuhama kwa staili ya kutoroka na deni letu ndipo tulipoenda
 wanawake wane na kumshushia kipigo” Alisema dada huyo
Baada ya taarifa hizo Shilole 
alitafutwa kupita simu yake ya mkononi pamoja na kupita kwenye makoloni 
yake hakuweza kupatikani isipokuwa majirani mbalimbali walikili kutokea 
kwa tukio hilo la kufedhehesha kwa mwanamuziki huyo.
chanzo: http://zeddylicious.blogspot.com/2013/08/shilole-apewa-mkongoto-wa-nguvu-kisa.html
No comments:
Post a Comment