Shirika la habari la Reuters
limeripoti siku ya Jumatatu ya wiki hii kuwa iliyowahi kuwa ya kwanza
kabisa kutoa simu za kisasa 'smart phones' na kusoma barua pepe 'first
smartphones and email pagers' kampuni kubwa na maarufu sana ya simu,
BlackBerry (asili yake Canada) huenda ikajiweka sokoni
......SOMA ZAIDI....kuuzwa kufuatia
kudorora kwa mipango na matarajio yake na kujiuzulu kwa Prem Watsa,
mwenye kampuni yenye hisa kubwa, Fairfax Financial Holdings Ltd.
BlackBerry ilikuwa moja ya makampuni pendwa yanayofanya vyema kwenye masoko ya hisa lakini kinyang'anyiro cha Apple Inc na Google Inc kimeiacha kampuni hiyo iliyozinduka na kutoka BlackBery 10 kushindwa kufanya vyema.
Serikali ya Canada haijataka kujiingiza katika suala hilo moja kwa moja ingawaje wadadisi wa mambo wanasema huenda wakaiacha inunuliwe na makampuni ya nje ili kuvutia uwekezaji. Lakini imeelezwa pia kuwa huenda Serikali hiyo ikalazimika kuingilia kati endapo atajitokeza mnunuzi kutoka nchini China kwa hofu kuwa huenda wakatumia mwanya huo kuipeleleza Serikali na nchi hiyo, jambo ambalo hawangetaka kuingia gharama kulidhibiti.
Makampuni ambayo yametolewa tetesi kuwa huenda yakajitosa kununua BlackBerry ni pamoja na Microsoft Corp, Amazon.com Inc, Lenovo Group Ltd na kwa kipindi cha nyuma yaliwahi kutamkwa kuonesha nia makampuni ya HTC Corp na Samsung Electronics Co Ltd.
Ikiwa inataka kushikilia soko na kuendelea kukaa kileleni sawa na makampuni mengine, BlackBerry inabidi ijiweke vyema zaidi kupambana na ushindani wa si tu makampuni makubwa yanayofanya vizuri sasa, bali pia na ongezeko la yanayokuja kwa kasi, hata kutoka China -- Huawei Technologies Co Ltd na ZTE Corp.

No comments:
Post a Comment