facebook likes

Monday, August 5, 2013

NEYMAR ANAUGUA UGONJWA WA UPUNGUFU WA CHEMBE HAI NYEKUNDU ZA DAMU MWILINI - BARCELONA YATHIBITISHA

Barcelona imesema kwamba mshambuliaji wake mpya kutoka Brazil Neymar ameanza kuugua ugonjwa wa upungufu wa chembe hai nyekundu za damu (Anaemia), lakini ugonjwa huo hautomfanya asiendelee na mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya.

Timu ya madaktari wa mabingwa wa La Liga wamesema kwamba waligundua mpangilio usiofaa wa damu ambao unaathiri uzalishaji wa chembe hai nyekundu za damu wakati mshambuliaji huyo alipofanyiwa vipimo vya damu.

Neymar, ambaye alijiunga na Barcelona kwa ada ya uhamisho inayozidi £50million, ameanza matibabu maalum. 
Barcelona imeaambia Associated Press kwamba kutokana na upasuaji aliofanyiwa wiki kadhaa zilizopita wa tonsils umesababisha aanze kuugua Anaemia lakini tayari ameanza matibabu na jambo hilo halitomzuia kuendelea na mazoezi na wachezaji wenzake.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...