facebook likes

Monday, August 5, 2013

HILI NDO KANISA LILILOPO UBUNGO....AMBAPO MAJIRANI WAMEANDAMANA ILI KUPINGA KELELE ZINAZOTOKA NDANI YA KANISA HILO



 Wakazi wa Mabibo External  jijini Dar es Salaam wamekusanyika nje ya lango kuu la kuingia katika  kanisa la Victorious Living lilipo katika eneo hilo kuushinikiza uongozi wa kanisa kuweka vifaa maaalum   vya kuzuia kelele wakati wanapofanya ibada zao. 
 
Wakazi wa Tabata External wamekusanyika nje ya lango kuu la kuingia katika kanisa la Victory Living  lilipo katika eneo hilo kushinikiza uongozi wa kanisa
kuweka vifaa maaalum vya kuzuia kelele wakati wanapofanya ibada zao kutokana na kanisa hilo kutumia vyombo vyenye sauti kubwa ilihali kanisa hilo lipo katika makazi ya watu.
 
Wakizungumza nje la kanisa hilo waumini hoa wamesema hawana shinda na huduma zinazotolewa na kanisa hilo bali na namna ambavyo wanafungulia vyombo vya muziki kwa sauti ya juu na hivyo wanajikuta usiku mzima hawalali hasa wagonjwa.
 
Baadhi ya wakina mama  wanaoishi jirani na kanisa hilo wamesema watoto wao sasa wameanza  kuonyesha hali ya utofauti kutokana na ukweli kuwa usiku hawalali na mchana hawalali kutokana na makelele hayo na hivyo wanaziomba mamlaka huska zione nini cha kufanya.
 
Akijibu tuhuma  hizo mchungaji kiongozi wa kanisa hilo mchungaji John Saidi amekiri kuwepo na malalamiko ya siku nyingine kati yake na wananchi wa eneo hilo lakini amekuwa akijitahidi mara kwa mara kupata ufumbuzi wa kero hizo ikiwemo kufuta baadhi  ya huduma zinazotolewa kanisa lake, huku afisa mtendaji wa mtaa huo bw henry mtogo akikiri kupokea malamamiko ya wananchi hao.

CHANZO ITV

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...