
Ofisi zaidi ya 12 za mabalozi wa Marekani katika Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini zimefungwa. Hatua hiyo inafuatia serikali ya Marekani kusema Ijumaa kwamba inaamini kuwa al-Qaeda au kundi linaloshirikiana na al-Qaeda huenda likawa linapanga mashambulio.
Ubalozi wa Marekani mjini Kabul piya umefungwa kwa sababu ya ilani hiyo kuhusu usalama. Mataifa kadha ya Ulaya nayo yamefuata - Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zimesema kuwa balozi zao mjini Sanaa, Yemen, zitafungwa mwisho wa juma.
Chanzo - BBC Swahili
No comments:
Post a Comment