TUME ya 
Vyuo Vikuu nchini (TCU) imekataa kuyachagua majina ya wanafunzi 8,805 
walioomba kujiunga na masomo ya shahada ya kwanza katika taasisi za 
elimu ya juu nchini kwa mwaka wa masomo 2013/2014 kutokana na sababu 
mbalimbali zilizojitokeza kwenye fomu zao za maombi.
hdg
Kwa 
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mtendaji wa TCU Profesa Sifuni 
Mchome, wanafunzi hao hawakuchaguliwa na tume hiyo kujiunga na vyuo 
vikuu kutokana na maombi yao ya programu zote walizochagua kushindwa 
kukidhi vigezo vilivyowekwa.
Ilieleza 
taarifa hiyo kuwa sababu za kutochaguliwa kwa wanafunzi hao ni pamoja na
 ushindani wa wanafunzi katika programu walizochagua, wanafunzi 
kushindwa kuwasilisha programu walizochagua na kuchangua programu ambazo
 hawana sifa nazo.
Hata 
hivyo, taarifa hiyo imewapa nafasi nyingine wanafunzi hao kuomba tena 
kwa awamu ya pili kwa kuchagua programu nyingine ambazo wana sifa nazo 
kupitia mfumo wa udahili wa TCU ambao umeshafunguliwa tangu Julai 29 
hadi Agosti 9 mwaka huu utakapofungwa.
Kwa 
mujibu wa taarifa hiyo, mwanafunzi anatakiwa kuangalia jina lake katika 
orodha ya wanafunzi ambao hawakuchaliwa na TUC, orodha inayopatikana 
kwenye tovuti ya taasisi hiyo ya www.tcu.go.tz na kufuata utaratibu 
uliowekwa kuomba upya.
"Baada ya
 mwanafunzi kuthibitisha jina lake kwenye orodha ya wanafunzi ambao 
hawakuchaguliwa iliyoko kwenye tovuti ya TCU, unatakiwa kufuata masharti
 yafuatayo, chagua program moja tu kutoka kwenye orodha ya programu 
inayopatikana kwenye tovuti ya TCU" alisema sehemu ya taarifa hiyo.
Kwa 
mujibu wa masharti hayo, pia mwanafunzi anatakiwa kufungua muongozo wa 
udahili unaopatikana kwenye tovuti hiyo na kuthibitisha kwamba anayo 
sifa stahiki ya kujiunga na programu aliyoichagua.
Masharti 
hayo pia yanamtaka mwanafunzi ambaye hakuchaguliwa, kuingia kwenye 
sehemu ya taarifa za mwanafunzi (profile) kwa kuingiza jina analotumia 
na namba yake ya siri, kubofya kitufe cha kuomba, kuchagua programu moja
 tu, kubofya kwenye makasha ya kuthibitisha na hatimaye kuwasilisha 
maombi yake.
"Baada ya
 kuwasilisha maombi yako mfumo wenyewe utakutaarifu kuwa ama unastahiki 
kuomba programu hiyo au la, na uchaguzi utaegemea kwenye msingi wa wa 
kwanza ndiye atakayehudumiwa mwanzo"ilisisitiza sehemu ya taarifa hiyo 
na kuongeza kuwa:
"Pindi 
programu moja itakapojaa, haitaoneshwa kwenye orodha ya programu 
zinazohitaji kujazwa kwenye mfumo wa udahili, hivyo utahitajika kujaza 
programu nyingine"
Kwa 
mujibu wa taarifa hiyo, mwisho wa kutuma tena maombi hayo ni Agosti 9 
mwaka huu na iwapo mwanafunzi atapata tatizo kuhusu maombi hayo 
atatakiwa kuwasiliana na TCU kwa anuani au kupiga simu namba 0757 
593868; 0757 594087; 0656 596822 na 0682 544832 au afike kwenye ofisi za
 tume zilizoko Mikocheni jijini Dar es Salaam.
mwisho
No comments:
Post a Comment