Mtandao wa Jambo umeripoti kwamba baadhi ya Makatibu wakuu wa Wizara na wajumbe wa kamati mbalimbali za katiba nchini Kenya, wamekiuka mpango wa Serikali kupunguza matumizi kwa kununua magari ya kifahari yakiwemo ya aina ya Limosine jambo ambalo limefanya Hazina kuwapa Onyo zito.
Taifa
la Kenya lilipata taarifa kwamba viongozi kadhaa wa juu wamenunua
magari 30 aina ya Mercedez Benz ndani ya mwezi mmoja ambapo wengine
wamedaiwa kujichukulia magari ya ulinzi kinyume na taratibu.
Unaambiwa
katibu mkuu wa Hazina Henry Rotich jumapili iliyopita aliliambia gazeti
la The Daily Nation kwamba taifa halitavumilia matumizi ya anasa na
ufisadi ambapo Wizara yake haijapitisha matumizi ya magari ya kifahari.
No comments:
Post a Comment