Na Gustav Chahe, Mufindi( Kamanda wa matukio)
MAHAKAMA
ya Wilaya ya Mufindi imetupilia mbali mashtaka yaliyokuwa
yakiwakabili Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) Hamad Yusuph na wenzake 42.
Kiongozi
huyo pamoja na wenzake walikuwa wakikabiliwa na makosa matatu likiwemo
la kufanya mkutano bila kibali pamoja na kuharibu mali ambazo ni kofia
za pikipiki (helmenti) 2 za polisi katika tukio lililosababisha kuuawa
aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel Ten
Daudi Mangosi katika kijiji cha Nyololo wailayani Mufindi.
Kutokana na tuhuma hizo Chadema iliweka pingamizi za kutaka kesi hiyo ifutwe kwa kuwa ilifunguliwa kinyume cha sheria.
Wakili
wa Chadema Lugaziya akisaidiana na mwanasheria wa Chadema Luka Sinkala
Mwenda waliweka pingamizi kuwa aliyetoa amri ya kusitisha mkutano na
kusababisha kifo cha mwandishi wa habari huyo ni kamanda wa Polisi
Michael Kamuhanda ambapo aliingilia kazi ya OCD wa Mufindi kwa kuwa
hakupaswa kutoa amri hiyo, kwamba wakati amri ya kusitisha mkutano
ilitolewa wakati hakukukuwa na vurugu na polisi walipiga mabomu wakati
watu wanatawanyika.
Pingamizi
zingine ni kwamba aliyetoa amri ya kutawanya mkutano hakuwa na cheo
chochote.Wakati Chadema ikizuiliwa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika
jimbo la Bububu Zanzibar walikuwa na mkutano wa kampeni za uchaguzi..
Polisi walisema wanazuia mkutano kwa kuwa sensa inaendelea wakati huo
sheria ya uchaguzi haizuii shughuli zingine kufanyika na kwamba walitaka
polisi waeleze sheria ya sensa inayozuia shughuli zingine kufanyika
inatoka wapi...
Watuhumiwa walipoambiwa watawanyike walitawanyika bila
kugoma na mkutano uliofanyika ulikuwa wa ndani kwa kuwa ulikuwa ukifanyika
ofisini baada ya mkutano wa hadhara kusitishwa na kwamba watuhumiwa
waliofikishwa mahakamani walikamatwa nje ya eneo la tukio kwa kuwa
walikuwa wametii amri.
Watuhumiwa
hao walikamtwa maeneo ya Igawa mpakani mwa Mkoa wa Iringa na Mbeya
baada ya kutoka katika eneo waliloamriwa kutawanyika.
Akitupilia
Mbali kesi hiyo, Hakimu wa Wilaya ya Mufindi D. Nyakunga alisema
pingamizi zilizowasilishwa na Chadema hazikujibiwa hata moja na upande
wa utetezi.
"Hakuna
pingamizi yoyote iliyojibiwa na upande wa utetezi. Hayo ni matumizi
mabaya ya kifungu namba 91 kinataka upande wa utetezi kujibu pingamizi.
"Pia ni matumizi mabaya ya muda na fedha za serikali na walipa kodi. Kwa sababu hizo, kesi hii inafutwa" alisema Nyakunga.
Naibu
Katibu Mkuu wa wa Chadema Zanzibar Hamad Yusuph na wenzake walifunguliwa
kesi hiyo baada ya kukamatwa wakati wa ufunguzi wa matawi Septemba 2,
2012 ambapo Mwangosi aliuawa na polisi kwa kupigwa bomu.
Credit: Kamanda wa Matukio
Credit: Kamanda wa Matukio
No comments:
Post a Comment