facebook likes

Wednesday, July 3, 2013

MACHANGUDOA WALALAMIKA UKATA MKUBWA ZIARA YA OBAMA, WASEMA MATEGEMEO YAO ILI KUWA NI KUWA MAMILIONEA.WASEMA AFADHALI UJIO WA BUSH ULIKUWA NA NEEMA NYINGI.

Rais Barack Obama wa Marekani

Polisi wa Kimarekani waliokuwa mwiba mkali kwa ulinzi wa Obama

Machangudoa wakiwinda wazungu maeneo ya Oysterbay Karibu na Ubalozi wa Marekani


Machangudoa wakiwa kazini

Katika hali ilisiyokuwa ya kawaida wakina dada maarufu wanaojihusisha na biashara ya kuuza miili yao maarufu kwa majina ya machangudoa wameulalamikia ujio wa Rais Barack Obama kwa kile kilichodaiwa haukuwa na faida yoyote kwa kukosa dili za pesa.

Wakiongea na blog hii kwenye baadhi ya sehemu wanazopatikana wakina dada hao walisema kuwa” Tumesikitishwa sana na ujio wa Obama kwani tulikuwa tumejipanga kupiga hela ndefu sana lakini patupu kwani watu wake tuliokuwa tumewategemea kuwanasa walikuwa busy na usalama pia kukaa kipindi kifupi kumechangia sisi kukosa mapato" Walisema wakina dada hao waliokutwa maeneo ya Coco Beach

Aidha machungudoa hao waliongeza kusema kuwa kipindi cha Bush ambae alikaa nchini karibu wiki moja walinufaika sana ambapo wengi wao walijenga majumba kwa pesa za ziara ya Bush kwani walifanikiwa kuwanasa watu wake na kufanya nao biashara kwa bei nzuri.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...