facebook likes

Wednesday, July 3, 2013

YALIYOJIRI KATIKA MKUTANO WA GEORGE BUSH NA WAKE WA MARAIS



Rais Jakaya Kikwete akiwa na Mke wake Mama Salma Kikwete wakizungumza na Rais Mstaafu wa Marekani Mheshimiwa George Bush wakati wa kikao cha wake wa Marais wa Afrika kinachofanyika katika hoteli ya Serena hapa Dar es Salaam.
 Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Rais Mstaafu wa Marekani Mheshimiwa George Bush muda mfupi kabla ya kuhudhuria ufunguzi wa mkutano wa wake wa Marais wa Afrika unaofanyika Serena hotel.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Rais Mstaafu wa Marekani  Mheshimiwa George Bush wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wake wa Marais na wakuu wa nchi za Afrika unafanyika Dar es Salaam kwa ufadhili wa Taasisi ya George Bush.  
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Rais Mstaafu wa Marekani  Mheshimiwa George Bush na baadhi  ya wake wa marais na wakuu wa nchi za Afrika  muda mfupi kabla ya Rais Kikwete kuufungua rasmi mkutano huo kwenye hoteli ya Serena.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (kkulia) Mke wa Rais wa Marekani, Michelle Obama (katikati) na Mke wa Rais Mstaafu wa Marekani, Mama Laura Bush, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wake wa Marais barani Afrika unaofanyika kwenye hoteli ya Serena.

======== =========  =========

MAMA OBAMA AMPONGEZA MAMA KIKWETE KWA KAZI KUBWA ANAYOFANYA YA KUWASAIDIA WATOTO WA KIKE

Mke  wa Rais  wa Marekani  Mama  Michelle Obama amempongeza  Mke wa Rais  Mama  Salma  Kikwete  kwa kazi  kubwa anayoifanya  ya kutoa elimu bure  kwa watoto Wa kike ambao ni yatima  na wanaoishi katika mazingira hatarishi .

Mama Obama  alizitoa pongezi hizo jana  wakati wa majadiliano baina yake na Mama Laura Bush kwenye mkutano wa   wake Wa Marais Wa afrika unafanyia katika hoteli ya Serena  jijini Dar es  Salaam.

Mama Obama alisema kuwa wake Wa Marais wanakazi kubwa ya kuhakikisha kuwa wanawasaidia  wanawake na watoto hasa katika upatikanaji Wa elimu na mahitaji mengine muhimu.

"Juzi nilitembelea  makumbusho ya taifa, nilikutana na watoto  ambao  baadhi yao walikuwa ni wale wanaosomeshwa na Mama Kikwete , niliongea nao watoto hawa wanapatiwa bure elimu, chakula na maladhi hakika nampongeza sana kwa kazi nzuri anayoifanya", alisema Mama Obama.

Akiongea wakati wa ufunguzi wa mkutano huo Mama Kikwete alisema kuwa wake wa Marais waliohudhuria mkutano huo wanawawakilisha wanawake wa Afrika  ambao wanahitaji kusaidiwa katika mambo ya afya,  elimu na ujasiriamali.

Mama  Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA)  alisema kuwa katika mkutano huo washiriki watapata nafasi ya kubadilishana ujuzi wa kazi  na kutembelea hospitali ya Kansa ya Ocen Road,kituo cha Mabinti na hospitali ya CCBRT ambako watajionea jitihada kubwa zinazofanywa na watanzania za kuisaidia jamii inayowazunguka.

Alisema kuwa baada ya kumalizika kwa mkutano huo anaamini kuwa washiriki watarudi katika nchi zao na kuweza kukubaliana na Serikali zao pamoja na wadau Wa wengine kuwekeza zaidi kwa wanawake ili kuimarisha bara  la Afrika.

Mkutano huo wa siku mbili   umeandaliwa na Taasisi ya Rais mstaafu wa Marekani George Bush na kuhudhuriwa na baadhi ya wake Wa Marais wa Afrika na Mke wa Waziri mkuu mstaafu Wa Uingereza Cherie Blair.

Mada kuu ni wekeza kwa wanawake imarisha Afrika lengo l ikiwa ni kuimarisha upatikanaji wa Afya  kwa wanawake, upatikanaji Wa elimu na uchumi katika Afrika.

Credit: Michuzi.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...