Klabu ya Chelsea imefikia makubaliano rasmi ya kumsajili nyota wa
timu ya taifa ya Uholanzi kwa vijana wenye umri chini ya miaka 21 Marco
Van Ginkel toka klabu ya Vittesse Arnherm . Nyota huyo atathibitishwa
kuwa mchezaji wa Chelsea ndani ya siku chache zijazo baada ya ofa toka
kwa The Blues ya Euro milioni 10.5 kukubaliwa na klabu ya Vittesse.
Usajili wa Van Ginkel utakamilika baada ya mchezaji huyo kufaulu
vipimo vya afya pamoja na makubaliano binafsi baina yake na Chelsea vitu
ambavyo kuna uhakika kuwa havitamzuia nyota huyo kuwa mchezaji mpya wa
Chelsea .
Kiungo mshambuliaji huyo aliibuka na kutengeneza vichwa vya habari
baada ya kufanya vizuri kwenye msimu wake wa kwanza kwenye klabu yake
ambapo alifuga mabao nane kabla ya kufanya vizuri kwenye fainali za
Mataifa ya Ulaya kwa vijana wenye umri chini ya miaka 21 na kabla ya
hapo alipewa tuzo ya ‘mchezaji mwenye kipaji bora wa mwaka” yaani Talent
Of The Year kwenye tuzo za wachezaji bora wa uholanzi kwa msimu
ulioisha jambo lililomfanya kocha wa timu ya Taifa ya wakubwa Louis Van
Gaal kumuita kwenye kikosi chake ambapo amecheza mechi moja .
Klabu ya Chelsea imepata wepesi wa kumsajili Marco Van Ginkel
kutokana na mahusiano mazuri yaliyopo baina ya klabu hiyo na klabu ya
Vittese Arnherm ambapo siku za nyuma Chelsea imewahi kuwapa Vittese
wachezaji ambao walicheza kwenye klabu hiyo kwa mkopo kama Gael Kakuta
na Patrick Van Aanholt.
Van Ginkel anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na Chelsea chini ya
utawala wa kocha mpya aliyerejea kwa mara ya pili Jose Mourinho baada ya
Andre Schurle toka Ujerumani huku wachezaji wengine kama Edinson
Cavanni na Wayne Rooney wakihusishwa na usajili ndani ya Chelsea.
No comments:
Post a Comment