facebook likes

Wednesday, July 3, 2013

WADUNGUAJI"SNIPPER" WA OBAMA WALIVYOKUWA VIVUTIO KWENYE MAGHOROFA YA POSTA, WENGINE KIBAO WALIKUWA KIGAMBONI LAKINI WALIKUWA WANAONA KILA KINACHOENDELEA MJI MZIMA!

 
Mmoja wa Wadunguaji ambae alionekana kwenye maghorofa ya Posta juu akiimalisha usalama.
 Madunguaji ambae alionekana kwenye vichaka huko Kigamboni akiimaRisha usalama kwa kutumia viona mbali ambavyo vilimuwezesha kuona kila kitu hasa maeneo ya Ikulu.

 Hii ni silaha maalum kwa ajili ya kudungua mtu mwenye umbali mrefu kupita maelezo ambapo inadaiwa uwezo wa kumtungua adui aliyekuwa kwenye umbali kati ya Mwenge na Kariakoo.
 Kazi ilikuwa moja tu kuseti mitambo kama Magaidi wangethubutu kufanya fyoko basi shughuli wangeiona kudadeki!!


 Mdunguaji huyu ambae nae alikuwa tayari kwa lolote kama ingetokea ambushi yoyote.

Hiyo ndo darubini iliyopo kwenye bunduki ya kudungulia ambayo humsaidia mtumiani kumlenga adui na huwa haikosei ikifyatuliwa inamfikia mlengwa.

Kama hukubahatika kuona watu hawa ambao mara kadhaa tumekuwa tukiwaona kwenye sinema za waigizaji maalum wa Kimarekani kama vile Bruce Wills nk utakuwa umekosa uhondo wa aina yake kwani walikuwa vivutio vikubwa sana kwenye Jiji la Dar pamoja na viunga vyake.
blog hii ambayo ilikuwa imemwaga waanahabari wake waliobobea kufanya habari za uchunguzi walibahatika kuwanasa wadunguaji hao" Snipper" wakiwa wamejiachia kwenye majengo marefu wakiimarisha usalama.

Habari zaidi zilieleza kuwa wadunguaji hao hawakuwa Posta peke yake bali kwenye mji mzima wa Dar ambapo Maghorofa yote ya Kariakoo yalijaa wao huku Kigamboni ndo wakiwa wale wenyewe wa kivita kabisa hali ilizusha hofu na mashaka tele kwa wananchi waliwaona.
Hata hivyo kifaa  kilichofungwa kwenye bunduki hizo ambacho humuwezesha mtumiaji kumlenga vyema mlengwa wake na inasemekana vinauwezo wa kufika kilomota kumi umbali wa kutoka Mwenge na Kariakoo.
Habari zaidi zilieleza kuwa wadunguaji hao walifika kwenye sehemu hizo siku tatu kabla ukiacha wale FBI ambao inadaiwa walikuja mwezi mmoja kabla.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...