facebook likes

Wednesday, August 21, 2013

WAKATI BONGO BADO KUKIWA NA UTATA - LIGI YA NIGERIA YAUZA HAKI ZA MATANGAZO YA TV KWA SUPERSPORT KWA $34 MILLION


Wakati Tanzania tukiwa kwenye sakata la uuzaji wa haki za matangazo yaTelevison,  wenzetu wa Nigeria wamesaini mkataba wa mamilioni ya dola.
SOMA ZAIDI.......Kwa mujibu wa ripoti kutoka nchini Nigeria, ligi kuu ya Nigeria imeingia mkataba wa miaka minne na kituo cha Televison cha Supersport.

Dili hilo, ambalo lilisainiwa katika ofisi za Supersport nchini Nigeria - limeiwezeshaLeague Management Company (LMC) ya Nigeria kuingiza jumla ya US$34 million.

Makubaliano hayo bado hajathibitishwa rasmi na Supersports lakini kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Nigeria ni suala la muda tu kabla dili hilo halijatangazwa rasmi kwenye vyombo vya habari.

Mkataba huo unategemea kuanza kwenye msimu wa 2015-16.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...