Wakati
polisi mkoani Kilimanjaro wakitangaza kuwashikilia watu watatu kwa
tuhuma za mauaji ya bilionea wa madini ya Tanzanite, Erasto Msuya (43),
pia wamesema mauaji hayo ni ya kulipiza kisasi katika biashara ya
madini.
SOMA ZAIDI....... Kauli
hiyo ilitolewa mjini hapa jana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Kilimanjaro, Robert Boaz, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari
juu ya hatua waliyofikia katika kusaka waliohusika na mauaji hayo ambayo
yalitetemesha miji ya Arusha na Moshi.
Kamanda wa polisi mkoa wa kilimanjaro Robert Boaz
Msuya
aliuawa saa 6:30 mchana kwa kupigwa risasi kando ya barabara kuu ya
Arusha – Moshi eneo la Mijohoroni, wilayani Hai karibu na Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), Agosti 07, mwaka huu na kufa
papo hapo.
No comments:
Post a Comment