facebook likes

Wednesday, August 21, 2013

CHONDE CHONDE JAMANI MWANANGU HAJANYONGWA: MAMA WA BINT KIZIWI ALALAMA,AMTUPIA LAWAMA NZITO RAFIKI NA MWANAE KWA KUMFUNDISHA KAZI HIYO HARAMU!


   Mama mzazi wa Binti Kiziwi, Rehema Selemani mkazi wa Sinza Kijiweni jijini Dar.
SOMA ZAIDI....
 
                 Sandra Khan maarufu Binti Kiziwi.
  
 Mama huyo aitwaye Rehema Selemani mkazi wa Sinza Kijiweni jijini Dar, amesema kuwa mwanaye amefungwa miaka mitatu na nusu na anawasiliana naye kwa njia ya simu kila baada ya miezi miwili.
“Taarifa za mwanangu kunyongwa si za kweli bali amefungwa miaka mitatu na nusu,” alisema mama huyo.
Mama huyo amemtupia  lawama rafiki wa karibu wa Binti Kiziwi aliyemrubuni kufanya biashara hiyo ya kusafirisha madawa ya kulevya.
 
 “Sikuijua safari hiyo ya mwanangu ila nilipigiwa simu na rafiki yake wakiwa wameshafika Nairobi, Kenya,” alisema.
Kama vile haitoshi, mama huyo anamlaumu rafiki kwa kuchukua dola 5,000 za mwanaye alizokutwanazo wakati akikamatwa.
Mbali na kuwasiliana na mwanaye, mama huyo amesema Binti Kiziwi amekuwa akimtumia fedha licha ya kwamba yuko gerezani.
“Ananitumia fedha, anasema kuwa huwa wanafanya kazi wakiwa gerezani na kulipwa,” alimalizia.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...