Raia mmoja wa Saudi Arabia mwenye uzito wa kilo 610 amelazimika kuchukuliwa kwa ndege kupelekwa hospitali baada ya kushindwa kutoka chumbani kwake kwa muda wa miaka miwili na nusu.
Jamaa huyo Khalid Mohsin Shaeri mwenye umri wa miaka 20, amesafirishwa kutoka mji wa kusini wa Jazan kupelekwa hospitali mjini Riyadh kwa maagizo ya Mfalme Abdulla wa Saudi Arabia.
Mpango wa kumuokoa ulilazimika kusubiri kwa miezi 6 mpaka kitanda maalum kilipotengenezwa nchini Marekani.
Wizara ya Afya ya Saudi Arabia imeshirikiana na idara ya usalama wa raia na Chama cha Msalaba Mwekundu cha Saudi kupanga namna ya kumtoa jamaa huyo baada ya kulamika kuvunja sehemu ya nyumba yake ili aweze kutolewa kutoka gorofa ya pili mpaka chini.
Ilibidi kutumia gari maalum la kunyanyua mizigo kumbeba Shaeri hadi kwenye gari la wagonjwa na kisha kupelekwa kwenye ndege iliyokuwa inamsubiri.
Waziri wa Afya nchini humo Dkt. Abdullah al Rabeeah akiita kitendo alichokifanya Mfalme Abdulla kuwa ni ishara ya ubinadamu.
Shaeri ambaye ana uzito sawa na watoto wawili wa Tembo au watu nane wa wastan, ameripotiwa kuwa ana kaka na dada ambao pia wanauzito na unene kupindukia lakini wanaweza kutembea.
No comments:
Post a Comment