Mwanaume
aliyetajwa kwa jina moja la Temba, mkazi wa Kimara-Rombo, Dar ambaye ni
dereva wa daladala amefumaniwa laivu na mkewe akiwa gesti na binti yao
wanayemlea.
SOMA ZAIDI..........
Tukio
hilo la aina yake lilijiri wiki iliyopita kwenye gesti hiyo iliyopo
maeneo hayohayo ya Kimara-Rombo, majira ya saa 10:00 jioni ambapo Temba
ambaye ni dereva wa daladala inayofanya safari kati ya Kimara na
Kariakoo alinaswa kiulaini baada ya kuwekewa mtego.
Baada
ya mke wa Temba kuweka mambo vizuri aliitaarifu wanahabari ambapo
alihojiwa maswali muhimu kisha kutakiwa kuwajulisha polisi ili
kuhakikisha kuna usalama wa kutosha.
Kwa
mujibu wa mke wa Temba, siku kadhaa nyuma aligundua kuwepo kwa
mawasiliano ya kimapenzi kati ya mumewe na binti yao hivyo akalazimika
kufanya uchunguzi wa kina.
Mama
Temba alisema kuwa katika harakati zake, siku ya tukio alifuma ujumbe
wa simu ‘SMS’ kwenye simu ya binti huyo, aliposoma alishtuka kuona
ujumbe wa kimapenzi kutoka kwa mumewe.
Kwa kuwa hakuamini alichokisoma, mama Temba ilibidi amwite binti yake ili amweleze vizuri juu ya ujumbe huo.
Alisema
kuwa binti huyo (jina linahifadhiwa) mwenye umri chini ya miaka 18,
hakuwa na hiyana alimweleza ukweli juu ya tabia ya baba yake huyo
kumtaka kimapenzi.
Aliendelea kusema kuwa alipombana kujua kama ‘walishaduu’, binti huyo alidai kuwa amekuwa akimtolea nje.
Mama
huyo alisema kuwa hakuwa na papara mara baada ya kuambiwa taarifa hizo,
alichokifanya alimtaka binti yake huyo amkubalie na amwambie baba yake
huyo wapange wakutane wapi.
Mama huyo alijifanya binti yake na kuanza kuchati na mumewe masuala ya mapenzi bila kufahamu kuwa anachati na mkewe.
Katika
kuchati, Temba alituma SMS: “Tulia natafuta mtu wa kumwachia gari
(daladala) halafu nitakutumia SMS kukuambia tukutane wapi, leo nataka
nifungue ukurasa wa mapenzi na wewe, mwanangu nakuhakikishia utakuwa na
maisha mazuri sana.”
Baada
ya kukubaliana kukutana gesti hiyo, mama huyo alikwenda kutoa taarifa
katika kituo kidogo cha polisi kilichopo maeneo hayo ya Kimara-Rombo na
kupanga jinsi ya kumnasa.
Majira
ya saa 10: 00 jioni, Temba alipata mtu wa kumwachia daladala na kutinga
katika gesti hiyo kisha kumtumia SMS binti huyo akimtaarifu ameshafika.
Tofauti
na alivyotarajia, ujumbe huo ulitua kwa mkewe ambaye alimwambia binti
huyo amfuate mara moja lakini ahakikishe ‘tunda’ halitafunwi.
Ilidaiwa
kuwa binti alipofika chumbani alimkuta mtu mzima akiwa amevaa taulo
tayari kwa kuvunja amri ya sita na binti yake huyo bila kujua kuwa nje
ya nyumba hiyo ya wageni kulikuwa na mkewe na polisi.
Ilisemekana
waliachiwa kama dakika kumi na tano ndipo timu nzima ya polisi
wakiongozwa na mkewe wakaingia ndani kwani hawakufunga mlango na
‘shughuli’ ilikuwa bado haijaanza.
Habari
zilisema kuwa mwanaume alipomuona mkewe anaingia chumbani akiwa
ameongozana na polisi nusura apasuke kwa mshtuko kwani alishindwa
kuyaamini macho yake.
Ilielezwa
kuwa mume alijaribu kutumia kila aina ya lugha kumuomba msamaha mkewe
lakini mke aliamuru askari kumtaiti kwa kumpiga pingu na safari ya
kwenda kituoni ikaanza.
Kabla
ya kupelekwa kituoni jamaa huyo aliibua timbwili zito na kusababisha
watu kukusanyika na kuongoza msafara kuelekea polisi huku akitembezwa na
taulo mtaani huku mkewe akimbebea nguo nyingine ikiwemo ‘boksa’.
“Yaani hata siamini, mume wangu nilimuamini sana kumbe ananizunguka,” alisema mke wa Temba kwa huzuni.
Alipofika
kituoni, Temba aliandikisha maelezo ambapo hadi mashushushu wetu
wanaondoka eneo hilo, kulikuwa na watu kibao waliokuwa wakipiga kelele
No comments:
Post a Comment