Sheikh Issa
Ponda Akiwa mahakamani mkoani Morogoro asubuhi ya leo Sheikh Ponda Amesomewa
Mashtaka Matatu
.....SOMA ZAIDI....
katika Mahakama ya mkoa wa Morogoro Likiwemo la uchochezi
alilolitoa Kwenye Mkutano wa Hadhara Tarehe 10 mwezi huu Ambapo Inadaiwa alisema kwamba ''Ndugu waislamu Msikubali
uundwaji wa kamati za ulinzi na usalama za Misikiti kwani kamati hizo zimeundwa
na Bakwata ambao ni vibaraka wa Serikali ''katika viwanja vya shule ya
kiwanja cha ndege Mkoani Morogoro.Baada ya kusomewa Mashitaka hayo Mahakama
imesema Upelelezi Umekamilikaa Dhamana Imefungwa na Amerudishwa Rumande
Mpaka tarehe 28 mwezi huu ambapo kesi hiyo itaanza kusikilizwa katika Mahakama
ya Mkoa wa Morogoro..
Sheikh Issa
Ponda Akiondoka mahakamani mara baada ya kusomewa mashtaka matatu na kesi yake
imehairishwa Hadi tarehe 28.08.2013
Ulinzi Ukiwa
umeimarishwa mahakamani leo
No comments:
Post a Comment