facebook likes

Monday, August 19, 2013

MOTO WAUNGUZA MITAMBO YA VODACOM.......!!


MOTO ulizuka juzi katika mitambo ya kuendesha mtandao wa Vodacom na kusababisha kukatika kwa mawasiliano.
....SOMA ZAIDI....Taarifa iliyotolewa na kampuni ya simu za mkononi Vodacom kupitia Ofisa Mkuu wa Mawasiliano, Georgia Mutagahywa ilisema moto huo uliozimwa, ulisababisha kusimama kwa huduma zote za kampuni hiyo. “Tunawaomba radhi wateja wetu wote kutokana na usumbufu wa kukosa mawasiliano uliosababishwa na kuungua kwa vifaa muhimu vya kuendesha mitambo yetu,” alisema Mutagahywa. Alisema, “Ninaomba niwahakikishie wateja wetu kwamba watarejeshewa huduma zote za vifurushi walizokuwa wamezinunua hapo jana pasipo kutakiwa kuzinunua upya pindi tutakapofanikiwa kurudisha huduma zote.” alisema Mutagahywa.

SOuRCE: HABARI LEO

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...