facebook likes

Monday, August 19, 2013

BBA Updates: Hawa ndio final 5 baada ya Bimp na Angelo kuondoka siku ya jana


 Siku ya jana (August 18) ilikuwa ni siku ya 84 tangu mashindano ya BBA kuanza na pia ilikuwa ni final eviction ambapo Angelo (SA) na Bimp (Ethiopia) waliyaaga mashindano hayo, na kuwaacha top 5 ndani ya mjengo, na jumapili ijayo itakuwa ndio siku ya mwisho ya mashindano hayo.



Top 5 waliobaki
1.Delish (Namibia)
2.Elikem (Ghana)
3.Beverly (Nigeria)
4.Cleo (Zambia)
5.Melvin (Nigeria)
Washiriki Bimp wa Ethiopia na Angelo wa South Afika wameyaaga rasmi mashindano ya BBA‘The Chase’usiku wa jana baada ya kupigiwa kura nyingi za kutoka kwenye mjengo huo.

Bimp ndiye aliyekuwa wa kwanza kuitwa na mtangazaji wa BBA,IK akiwa mshiriki wa 21 kutoka The Chase na baadaye kufuatiwa na Angelo na kukamilisha idadi ya washiriki wawili waliaga mashindano hayo usiku jana Jumapili,Agosti 18.
Mshiriki kutoka nchini Na,ibia Dillish ambaye naye alikuwa kikangoni aliibuka kidedea baaya ya kunusurika kutoka kwa kupata kura nyingi baada ya kupigiwa kura na nchi saba huku Angelo na Bimp wakipigiwa na nchi nne.
Washiriki walioingia top 5 ni Dillish,Elikem,Beverly,Melvin na Cleo.

Angalia jinsi kura zilivyopigwa
Angola: Bimp
Botswana: Angelo
Ghana: Dillish
Kenya: Dillish
Ethiopia: Bimp
Malawi: Bimp
Namibia: Dillish
Nigeria: Dillish
South Africa: Angelo
Sierra Leone: Dillish
Tanzania: Bimp
Uganda: Dillish
Zambia: Angelo
Zimbabwe: Dillish
Rest of Africa: Angelo

Total: Dillish = 7, Angelo = 4, Bimp = 4.
(Total: 15 Votes)

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...