Jose Mourinho amesema Chelsea itasubiri kujua Wayne Rooney ataamua nini kuhusu hatma yake kabla hawajutuma ofa ya tatu kwa ajili ya kumsaini mchezaji huyo Manchester United .
The Blues tayari wameshashuhudia ofa zao 2 za mwanzo zikikataliwa na Red Devils - huku boss wa klabu hiyo David Moyes akisisitiza mchezaji huyo hauzwi.Chelsea wamekataa kukubali kushindwa, ingawa inaonekana wazi kuna uwezekano mkubwa mshambuliaji huyo mwenye miaka 27 ataendelea kuwepo Old Trafford.
Akiongea na waandishi wa habari baada ya mchezo dhidi ya United Mournho alisema: "Kwanza ningependa kusema.
"Hii klabu (Man United) ni special sana kwa sababu katika klabu yoyote duniani wakati mchezaji anapotaka kuondoka, huwa anakosa sapoti kabisa. Mchezaji anapotaka kuondoka anakuwa kwenye wakati mgumu sana, lakini hapa wamemsapoti Rooney muda wote.
"Nadhani hii klabu special sana, yenye mashabiki special pia, na ikiwa Rooney atafanya uamuzi wa kubaki, sisi tutakuwa wa kwanza kuheshimu uamuzi huo na kuachana na suala la kutaka kumsajili."
Alipoulizwa kama watatuma ofa mpya, Mourinho aliongeza: "Inategemea na uamuzi wa mchezaji, namna atakavyotaka, jinsi hisia zake zitakavyomtuma.
"Ikiwa sasa hataki kuondoka, basi sisi hatuna namna zaidi ya kuachana na suala la kumsajili. Tunahitaji kujua nini kitatokea."
No comments:
Post a Comment