Mwakilishi wa Jimbo la Kiembe Samaki Mkoa wa Mjini Magharibi-Zanzibar,Manzour Yusuf Himid amevuliwa uanachama na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa(NEC) akituhumiwa kushindwa kusimamia malengo ya CCM na kutekeleza masharti ya uanachama.
HII NDIO HISTORIA YAKE
MANSOOR Yussuf Himid ni mwanasiasa na mfanyabiashara aliyezaliwa tarehe 3 Novemba 1967 kisiwani Unguja. Alisomea masomo yake ya ya msingi na sekondari nchini India kati ya mwaka 1976 na 1987. Kabla ya kuzivaa rasmi siasa mwaka 2000 alipoteuliwa mjumbe kwenye Baraza la Wawakilishi, Mansoor alikuwa akijihusisha sana kwenye biashara ya hoteli.
Katika uchaguzi wa 2005 alichaguliwa mwakilishi wa jimbo la Kiembesamaki kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) nafasi ambayo ameishikilia hadi sasa.
Mansoor ni mwanachama mkereketwa wa CCM aliyeshikilia nafasi za juu za chama hicho. Amewahi kuwa mjumbe wa Kamati Tendaji Taifa (NEC) na Mweka Hazina wa Chama kwa upande wa Zanzibar kati ya mwaka 2002 na 2012.
Nje ya CCM, Mansoor ameshika nyadhifa mbalimbali za uwaziri katika Baraza la Mawaziri la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Kwanza kutoka mwaka 2000 hadi 2004, alikuwa Naibu Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi, halafu kati ya 2004 na 2010 alikuwa Waziri kamili kwenye wizara hiyohiyo. Baadaye kuanzia 2010 hadi 2012 alikuwa Waziri wa Kilimo na Rasilimali.
Mansoor alihudumu kama mjumbe wa Baraza la Biashara la Zanzibar baina ya mwaka 2002 hadi 2012.
Moja ya mambo yanayomtafautisha kiongozi huyu, ambaye ni mtoto wa Mkuu wa kwanza wa Jeshi la Zanzibar baada ya Mapinduzi, Brigadea Jenerali Yussuf Himid, ni kuthubutu kwake kusema anachokiamini na kukisimamia. Kwa mfano, amekuwa akisimama kidete kuhusu suala la Maridhiano ya Wazanzibari na Umoja wa Kitaifa. Akiwa mmoja wa wajumbe sita wa Kamati ya Maridhiano, alishiriki kikamilifu kuyaanzisha hayo maridhiano mwaka 2009.
Wajumbe wengine wa Kamati hiyo ni mwenyekiti wake Hassan Nassor Moyo (CCM), Eddie Riyami (CCM), Abubakar Khamis Bakari (CUF), Ismail Jussa Ladhu (CUF) na Salim Bimani (CUF).
Aidha, Mansoor amekuwa miongoni mwa Wazanzibari walio katika safu ya mbele kuutetea muundo wa Muungano utaoipa Zanzibar mamlaka yake kamili. Yote hayo yamemfanya ang’are machoni mwa Wazanzibari na awe kipenzi chao.

source:dj sek
No comments:
Post a Comment