facebook likes

Tuesday, August 27, 2013

BINTI APEWA KICHAPO JIJINI ARUSHA BAADA YA KUKATISHA MITAA AKIWA NUSU UCHI..

Msichana mmoja ambaye jina lake halikujulika amejikukuta katika wakati mgumu baada ya kuzomewa na   kuchapwa viboko na kundi la watu katika eneo la soko la nmc jiji arusha kwa madai ya kuvaa nguo fupi hali iliyowalazimu wasamaria wema kuingilia kati  na kutumia nguvu kubwa ili  kumwokoa na kumsitili kwa kumfunika na nguo zingine.  
SOMA ZAIDI...........
Watu walio shuhudia tukio hilo wamedai kuchukizwa na aina ya nguo alizizovaa msichana huyo ambazo haziendani na maadili ya Kitanzania, ndiyo maana waliamua kumwadabisha ili kukomesha tabia hiyo. 

Kwa upande wao wanawake walio msitili msichana huyo kwa kumpa nguo za heshima na kumhifadhi katika Gareji ya jirani kabla ya kumkimbiza kwa gari aina ya Toyota Hiace wamesema hawaridhishwi na tabia hiyo inayowazalilisha wanawake na kuwataka wasichana kuavaa nguo za kujisitili ili kujenga heshima katika jamii.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...