facebook likes

Tuesday, July 23, 2013

TIMU ZA NIGERIA ZILIZOVUNJA REKODI YA KUFUNGANA MABAO MENGI ZAFUNGIWA MIAKA 10 - WACHEZAJI, VIONGOZI NA MAREFA WOTE WALA VIFUNGO VYA MAISHA



Wachezaji na maofisa wa timu zilizohusika katika mechi mtoano ambazo ziliishia kwa matokeo ya 79-0 and 67-0 wamefungiwa kifungo cha maisha cha soka.
Plateau United Feeders walishinda 79-0 dhidi ya Akurba FC wakati Police Machine FC waliwafumua Bubayaro FC 67-0.
Klabu hizo nne zimefungiwa kwa miaka 10.
Shirikisho la soka la Nigeria (NFF) kupitia kamati yake ya nidhamu pia limetoa ushauri kwamba marefa waliohusika na michezo hiyo miwili inabidi wafungiwe maisha. 
Plateau United Feeders na Police Machine walienda kucheza mechi zao wakiwa sawa kwa pointi, na hivyo walikuwa wakigombania nafasi ya kupanda daraja.
Feeders ilifunga mabao 72 ya mabao yao katika kipindi cha pili, wakati Police Machine waliripotiwa kufunga mabao 61 baada ya mapumziko ya mchezo. 
Matokeo hayo yalimaanisha kwamba Plateau iliwazidi Police Machine kwa tofauti ya mabao.
NFF ilisema kupitia taarifa yake: "NFF wamekubali mapendekezo yaliyotolewa na watawasiliana na klabu, vyama vya soka vya kanda husika, CAF na FIFA.
"Tutatoa kwa kuchapisha majina ya wachezaji wote pamoja na maofisa kwa pamoja na picha zao na taarifa."

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...