Khalid Mohamed, Top In Dar (T.I.D)
ambae pia ni mmiliki wa Top Band amepinga vikali taarifa zinazoonesha
kuwa Nyimbo za msanii mwenzake Ali Kiba zinasikilizwa zaidi Muscat
huenda kuliko msanii mwingine wa Bongo Fleva.
Taarifa hizi
zilizotolewa na mtandao wa Bongo5 ambao ulipata maelezo ya kina baada ya
kuchat na mtanzania aishie nchini Muscat aliyetambulika kwa jina la
Rayya Al Habsi aliyewapa tathmini kuhusu nyimbo za kibongo
zinazosikilizwa zaidi huko mjini Muscat,Oman.
Rayya alisema
nyimbo za Ali Kiba zinasikilizwa sana lakini pia wasanii wengine
wanaopendwa ni Diamond Platinumz, Ommy Dimpoz na Dully Sykes.
Rayya
aitaja pia upande wa mduara kuwa ni AT, Off side Trick na Kilimanjaro
Band, na kwamba band inayofunika zaidi ni Twanga Pepeta.
Taarifa
hizi zinakuja wakati ambapo T.I.D amepata deal la kwenda mjini Muscat
kupiga show akiwa na band yake ‘Top Band’, na hivyo ameona kama taarifa
hizi zimepotoshwa na yeye ndiye alistahili kutajwa katika nafasi
aliyopewa ‘Ali Kiba.’ Na kwamba yeye ameshapiga show mara mbili na
anaenda kwa mara ya tatu akiwa na band yake.
Kupitia ukurasa wake wa facebook T.I.D a.k.a Mnyama amedondosha maelezo confidently.
“This
came after I have been mentioned perfoming well its too late for this
reminder its my time,and they listen to me alot its my third time
perfomin there and this time with my band.”
Kisha akaambatanisha
na kichwa cha habari chenye picha ya Ali Kiba kama kilivyoandikwa na
Bongo5, yenye kichwa cha habari “Nyimbo za Ali Kiba zinasikilizwa zaidi
Muscat ‘huenda’ kuliko msanii mwingine wa Bongo Flava.”
Well, yale
yanaweza kuwa ni maoni ya Rayya, maoni sio utafiti rasmi japo unatoa
picha ya jumla. Lakini inaonekana kama Top In Dar hataki kuwa Down any
where hivi hivi.
No comments:
Post a Comment