facebook likes

Tuesday, July 23, 2013

SKENDO: VYETI VYA SHULE YA MSINGI VYAONYESHA RADAMEL FALCAO NI MKUBWA ZAIDI ANAYOSEMA MWENYEWE

Profile ya Falcao inayonyesha na umri wa miaka 27 wakati ni 29.


Wakati masuala ya wachezaji wa soka kufoji vyeti vya kuzaliwa kuficha umri wao halisi ukiwa umewaandama wachezaji wa kiafrika, leo hii zimeibuka ripoti kutoka Amerika ya Kusini zikiripoti kwamba mshambuliaji wa kikorombia Radamel Falcao amefoji umri wake.

Kwa mujibu wa vyeti vyake vya shule ya msingi vinaonyesha nyota huyo wa Monaco amezaliwa mwaka 1984 na sio 1986 kama inavyoonekana kwenye wasifu wake. Falcao alianza kusoma kwenye shule ya msingi ya Colegio San Pedro Claver iliyopo kwenye mji wa Bucaramanga akiwa na miaka mitano mnamo mwaka 1989. 

Kwa maana hiyo Falcao amejipunguzia umri wa miaka 2 katika umri wake wa halisi ambao ni miaka 29 mpaka sasa. Tangu kuanza kusambaa kwa taarifa hizi sio mwenyewe mchezaji wala wakala wake ambaye ajitokeza hadharani na kukanusha.

Cheti cha shule ya Colegio San Pedro Claver kikiwa picha ya Radamel Falcao Garcia aliokuwa mtoto


Cheti cha shule ya msingi cha Bucaramanga

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...