Kufuatia kikao cha triple K (Kenyatta, Kagame na Kaguta (Mseveni)) kilichofanyika Kampala mwezi uliopita, jana bandari ya Mombasa wamefungua rasmi ofisi yao Kigali kwa ajili ya kuhudumia nchi za Rwanda, Burundi na DRC. Moja ya mambo waliyokubaliana triple K ni kuondoa matatizo yote yanayofanya biashara baina ya nchi hizi kuwa ngumu.
Sote tunafahamu mahusiano mabovu yaliyopo kati ya Rais Kikwete na Rais Kagame kwa sasa. Ni ukweli usiopingika kwamba kwa sasa Bandari ndio cash cow ya Tanzania, hakuna cha kilimo, madini, utalii au chochote utakachotaja. Kama kumbukumbu zangu bado ziko poa, bandari inaingiza over 50 bil kwa mwezi. Swali ninalojiuliza, hivi tumejipangaje ili kuwa competitive zaidi in case nchi hizi nne kwa maana ya DRC, Burundi, Rwanda na Uganda zitaamua kwa kiasi kikubwa kuanza kutumia bandari ya Mombasa? Think of hayo mapato niliyotaja, ajira, biashara za mafuta, hotel n.k.
No comments:
Post a Comment