facebook likes

Tuesday, July 23, 2013

Breaking News!!!! Malkia Elizabeth apata kitukuu.


Wazazi wapya..Prince William na Mkewe Kate Middleton.
Wazazi wapya..Prince William na Mkewe Kate Middleton.

Kate Middleton na msaidizi wake wakati anafanya shopping ya mtoto wake.
Kate Middleton na msaidizi wake wakati anafanya shopping ya mtoto wake.
Mke wa mjukuu wa Malkia wa Uingereza Kate Middleton amejifungua mtoto wake wa kwanza ikiwa imepita miezi zaidi ya 12 tangu alipoolewa rasmi kwenye familia ya kifalme.
Middleton na Mumewe ambaye ni mjukuu mkubwa wa malkia Elizabeth Prince Williams wameeleze furaha yao baada ya kupata mtoto huyo ambaye moja kwa moja anaingia kwenye kizazi cha Ufalme ambapo anakuwa mrithi wa tatu wa kiti cha Ufalme baada ya babu yake ambaye Prince ni Prince Charles na baba yake Prince William ambaye atarithi toka kwa Prince Charles.
Kate Middleton ambaye wadhifa wake rasmi ni “Duchess of Cambridge” alijifungua mtoto huyo kwenye hospitali ya St Marrys iliyoko eneo la Paddington . Hospitali hiyo ndipo alipoazaliwa baba mzazi wa mtoto huyo na Mume wa Katte Middleton ambaye ni mjukuu wa Malikia Elizabeth Prince Williams akizaliwa na Marehemu Princess Diana mwaka 1982.
Kate Middleton akifanyiwa vipimo vya nguo wakati alipokuwa mja mzito.
Kate Middleton akifanyiwa vipimo vya nguo wakati alipokuwa mja mzito.
Taarifa za kuzaliwa kwa mtoto huyo zimepokewa kwa furaha na wanasiasa mbalimbali duniani ambapo waziri mkuu wa Uingereza David Cameroon na Rais wa Marekani Barack Obama wameongoza orodhanya watu mashuhuri waliotuma salamu za pongezi kwa mtoto huyu mpya kwenye faimilia ya Malkia Elizabeth.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...