MSHAMBULIAJI nyota wa
klabu ya Borussia Dortmund, Robert Lewandowski ameahidi dhamiri yake ya
kujitoa kwa dhati kwa klabu hiyo pamoja na kushindikana kwa uhamisho
wake kwenda klabu ya Bayern Munich katika kipindi cha usajili wa majira
ya kiangazi. Lewandowski
ambaye mkataba wake na Dortmund unamalizika 2014 alikataa kusaini
mkataba mpya msimu uliopita akidai kuwa anategemea kuchagua klabu
atakayokwenda mapema. Baada
ya usajili kuanza na Lewandowski kutaka kuwa mchezaji wa pili
kuchukuliwa na mahasimu wao Bayern baada ya Mario Goetze, Dortmund
walizuia uhamisho wa nyota huyo ambao ungewaletea mamilioni ya euro. Lewandowski
alikaririwa na gazeti moja nchini Ujerumani akidai kuwa atajitoa kwa
nguvu zake zote kwa Dortmund haijalishi kitu gani kimetokea kwani
aanapokuwa uwanjani huwa hafikirii mambo hayo. Mshambuliaji
huyo wa kimataifa wa Poland alimaliza msimu uliopita vyema kwa kufunga
mabao 24 katika Ligi Kuu nchini Ujerumani na kuongeza mengine 10 katika
michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya yakiwemo mabao manne aliyofunga
katika mchezo mmoja dhdi ya Real Madrid.
No comments:
Post a Comment