Timu
hiyo yenye maskani yake, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam,
itaondoka na kikosi chake kizima kasoro wachezaji wawili tu majeruhi,
kiungo Mkenya, Humphrey Mieno na mshambuliaji Mganda, Brian Umony.
Meneja
wa Azam FC, Jemadari Said ametumbia asubuhi ya leo kwamba,
timu inaendelea na mazoezi kwenye Uwanja wake wa Azam Complex, Chamazi
kwa ajili ya safari hiyo, wakati majeruhi Umony na Mieno wanafanya
mazoezi ya gym.
Mshambuliaji
huyo wa zamani wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya Kariakoo United ya
Lindi, amesema kwamba timu ikiwa Afrika Kusini pamoja na kuweka kambi ya
mazoezi, pia itacheza mechi nne za kujipima nguvu dhidi ya timu kubwa
za huko.
Ingawa
bado ratiba ya mechi za Azam nchini humo haijajulikana, lakini
inafahamika miongoni mwa timu zitakazocheza na Azam ni Orlando Pirates,
Supersport United, Kaizer Chiefs na Mamelodi Sundowns.
Kuna uwezekano Azam ikacheza mechi zaidi kulingana na namna ambavyo timu zaidi nchini humo zitavuwiwa kucheza nayo.
Azam
inatarajiwa kurejea nchini siku moja kabla ya kucheza mechi ya kuwania
Ngao ya Jamii kuashiria kufungua pazia la msimu mpya wa Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Yanga SC, Agosti 17, mwaka huu Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Safari
hii Azam, washindi wa pili mara mbili mfululizo wa Ligi Kuu wamepania
kutwaa Ngao mbele ya Yanga, baada ya mwaka jana kufungwa na Simba SC na
kocha Muingereza Stewart Hall anajiandaa kikamilifu kwa ajili hiyo.
Azam wakijifua ufukweni |
source:binzubeiry
No comments:
Post a Comment