MBUNGE wa Jimbo la Kinondoni, jijini Dar es Salaam kwa tiketi ya
CCM, Idi Azzan, amejilisalimisha' polisi na kutaka jeshi hilo, kufanyia
uchunguzi tuhuma za kuhusishwa na biashara za dawa za kulevya na iwapo
itabainika anahusika, hatua za kisheria zichukue mkondo wake.
Mbunge huyo alifikia hatua hiyo jijini Dar es Salaam
jana baada ya barua zilizoandikwa na watu wanaodai ni wafungwa wa
Tanzania wanaotukia adhabu zao mjini Hong Khong, nchini China, kusambaa
kwenye mitandao ya kijamii zikimhusisha yeye (Azzan) kuwa amekuwa
akifanya biashara hiyo akiwatumia vijana hao. Wafungwa hao wanadaiwa
kuwa wanatumikia adhabu zao baada ya kupatikana na makosa ya dawa za
kulevya.
Mbunge huyo alisema alienda kutoa taarifa hizo mwenyewe Kituo Kikuu cha Polisi Kati, jijini Dar es Salaa.
"Nimeamua
kwenda kituo cha polisi kwa ajili ya kutoa taarifa ili ufanyike
uchunguzi wa jambo hilo na ukweli ubainika na hatua za kisheria zifuate
juu yangu," alisema Azza, wakati akizungumza na gazeti hili kwa njia ya
simu jana.
Azzan alibainisha kuwa ameamua kwenda kutoa taarifa
polisi ili waanze uchunguzi wao. Alisema barua hizo ambazo hazina anuani
ya eneo zilipotoka wala majina ya waandishi wake zina lengo baya dhidi
yake na kutaka kuposha umma.
"Mimi sipo juu ya sheria itakapobainika najihusisha
na tatizo hilo, nichukuliwe hatua mara moja, na nitajiuzulu ubunge
wangu," alisisitiza Azzan na kuongeza;
"Wapiga
kura wangu wa Kinondoni pamoja na wananchi kwa ujumla inatakiwa waelewe
kuwa barua hizo zina nia mbaya zenye lengo la kunichafua na kama kweli
wana ushahidi wangetaja majina yao."
Mwishoni wiki hii katika mitandao mbalimbali ya
kijamii ziliwekwa barua zinazodaiwa kuandikwa na wafungwa waliokamatwa
na dawa za kulevya nchini China zikimhusisha mbunge huyo na biashara
hiyo.
Barua hizo pia zinawataja baadhi ya viongozi wa
serikalini kuwa wanajihusisha na mtandao wadawa za kulevya, lakini
hazikuainisha majina yao.
No comments:
Post a Comment