facebook likes

Wednesday, June 26, 2013

THEO WALCOTT AFUNGA NDOA NA MPENZIWE TOKA UTOTONI NCHINI ITALY

Siku ya Jana Mchezaji mpira wa Ligi kuu ya uingereza chini ya timu yake Arsenal
aliamua kukacha ukapela na kufunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu toka utotoni
aitwae Mellanie...!!

Harusi hiyo iliyoudhuriwa na watu wengi maarufu na hata wachezaji wenzake kutoka
arsenal na wengine,waliomba kuleta zawadi yoyote kwenye harusi baadala
yake Walcott aliomba wachangie mfuko wa Willow
Foundation unaosimamia maswala ya magonjwa ya kansa,
 unaosimamiwa na mkongwe wa zamani
wa Arsenal Bob Wilson.....Azima hiyo imekuja baada ya dada wa mkewe na Walcott
kufariki akiwa na Umri wa Miaka 16 kwa matatizo ya kansa ya Ini....
Baadhi ya wachezaji wa Arsenal walioudhuria harusi hiyo walikuwa,
Alex Oxlade Chamberlain aliesafiri na Jet mpaka Italy,Aaron Ramsey,
Kieran Gibs,Thomas vermaelen......!!
 Ndoa hiyo iliyofanyika kwenye kasri kubwa ya kifahari nchini Italy
iliudhuriwa na wageni waalikwa na aikutangazwa popote kabla ya ndoa...!
Ilianzia zamani,Picha hii ni mwaka 2006 Theo walcott akiwa na mpenzi wake kwenye
Uzinduzi wa Harrypotter jijini London...!!
Theo walcott kwenye mikiki mikiki uwanjani kwenye moja
 mechi za ligii kuu Uingereza...

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...