facebook likes

Wednesday, June 26, 2013

Man City na Juventus zafikia makubaliano juu ya usajili wa Carlos Tevez.

image

Mabingwa wa ligi kuu nchini Italia Juventus wanakaribia kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa toka nchin Argentina Carlos Tevez baada ya kufikia makubaliano na klabu yake ya sasa Manchester City .
Juve wamekubali kulipa ada ya uhamisho ya Paundi milioni 27 kwa ajili ya Mshambuliaji huyo na Man City imeridhia kumuuza kwa Juventus . Usajili huo utakamilika baada ya mshambuliaj huyo kufanyiwa vipimo vya Afya nchini Italia ndani ya siku chache zijazo.
Viongozi wa klabu zote mbili wamekuwa kwenye mazungumzo yaliyodumu kwa muda wa siku mbili na Tevez pamoja na wawakilishi wake wanatarajiwa kusafiri hadi nchini Italia baadaye hii leo ( jumatano) ambako watafanya mazungumzo yahatua za mwisho ikiwemo kufikia makubaliano juu ya masuala binafsi ya Tevez ukiwemo mshahara na bonus nyinginezo.
Ada ya uhamisho ambayo Juve wanailipa City kwa ajili ya Tevez kimsingi  Paundi milioni 9 lakini inatarajiwa kupamda hadi kufikia paundi milion 27 baada ya kuongezeka kwa bonus pamoja na idadi ya michezo atakayocheza akiwa na Juve pamoja na mafanikio atakayopata ndani ya msimu wake wa kwanza .
Akiwa na umri wa miaka 29 , Tevez anakuwa mchezaji wa kwanza mwenye jina kubwa kusajiliwa na Juventus msimu huu baada ya klabu hiyo kusaka mshambuliaji wa kiwango cha dunia kwa muda mrefu bila mafanikio.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...