Zikiwa zimepita saa karibu 24 tangu ilipotangazwa kuwa Bayern
Munich wamekamilisha usajili wa Thiago Alcantarra , Barcelona huenda
wakalazimika kupoteza mchezaji mwingine wa safu ya kiungo baada ya klabu ya Manchester United kutuma ofa ya kumsajili kiungo Cesc fabregas . United
wakiugulia machungu ya kumkosa Thiago wametuma ofa ya paundi milioni 26
kwa ajili ya Fabregas wakiwa kwenye harakati za kuimarisha kikosi chake
hasa nafasi ya kiungo ambayo kocha mpya David Moyes anaiona inahitaji
kuongezewa nguvu .
United baada ya kutangaza hapo jana kuwa wana fedha za kufanya
usajili wa nyota yoyote ambaye Moyes atamhitaji kwenye kikosi chake
walipata pigo la kwanza baada ya taarifa ya Thiago kwenda Bayern kutoka
rasmi baada ya mchezaji huyo kuripotiwa kuwa kwenye rada za David Moyes
ambaye amekuwa akimtazama kama mrithi wa muda mrefu wa kiungo Paul
Scholes ambaye amestaafu .
Usajili wa Fabregas hautakuwa rahisi kwani mchezaji huyo aliwahi
kuichezea Arsenal siku za nyuma na klabu hiyo (Arsenal) ina chaguo la
kwanza la kumsajili au kukataa kumsajili Cesc kwa mujibu wa mkataba wake
wakati alipouzwa toka Arsenal kwenda Barca misimu miwili iliyopita .
Ugumu mwingine unatokana na ukweli kuwa Fabregas ana nafasi ya kudumu
kwenye kikosi cha kwanza cha Barca na haitakuwa rahisi kwa klabu hiyo
kuruhusu kiungo mwingine kuondoka baada ya Thiago . Hata hivyo maisha ya
Fabregas tangu arejee Barca toka Arsenal hayajakuwa mepesi kama
ilivyotarajiwa na wengi na kocha aliyeondoka Pep Guardiola aliwahi
kupendekeza kuuzwa kwa mchezaji huyo baada kutoridhishwa na na kiwango
chake .
No comments:
Post a Comment