facebook likes

Tuesday, July 16, 2013

KIKOSI CHA KWANZA CHA WACHEZAJI WAHALIFU WA KISHERIA: MESSI, SUAREZ, DE GEA NA WENGINEO


Siku chache zilizopita mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kutuhumiwa kukwepa kodi. Alifunguliwa kesi lakini mwishowe akaamua kulipa kiasi cha $19m kumaliza kesi hiyo nje ya mahakama.

Makala hii inajaribu kupanga kikosi cha wachezaji ambao wameshawahi kutuhumiwa na makosa ya kisheria. Kinawahusisha wanasoka ambao wameshawah kutuhumiwa na kukutwa na hatia ya makosa ya ubakaji, wizi, na hata kupigana. 

Golikipa: David De Gea - Manchester United
 Mapema mwaka 2011, baada ya kukamilisha usajili wake wa kujiunga na United David De Gea alikutwa na tuhuma za kuiba maandazi katika supermarket ya Tesco. Alijitetea kwamba aliondoa kwenye supermarket na kuenda kwenye gari ili kufuata fedha za kulipa, lakini tayari taswira yake iliharibiwa na tuhuma hizo. 

Beki wa Kulia: Micah Richards - Manchester City. 
Huyu alikutwa na hatia ya kukimbia kulipa fedha za kupaki gari lake, pia alikutwa na makosa ya kuendesha gari kwa kasi sana. Kijana huyu anayelipwa mamilioni ya fedha na waarabu wa City kwa sasa anatumikia adhabu ya kutoendesha gari gari. 

Beki wa kati: Titus Bramble - Sunderland.

 Huyu inawezekana ni mmoja wa mabeki wabovu wa premier league, anatuhumiwa na kesi ya ubakaji. Yeyey na mdogo wake Tesfaye Bramble wote walithumiwa kumbaka msichana mmoja lakini kwa bahati nzuri kwake alikutwa hana makosa na mdogo wake akifungwa kwa kosa hilo. 

Beki wa kati: John Terry - Chelsea. 
Terry ametuhumiwa na makosa makubwa mawili. Alikutwa na hatia na FA kwa kosa la kumtukana kibaguzi Anton Ferdinand na alipewa adhabu ya kusimamishwa mechi kadhaa. Pia aliwahi kukiri kulala na mke wa mchezaji mwenzie wa Chelsea Wayne Bridge.

Beki wa kushoto: Danilo Larangeira - Udinese. 
Huyu ni mbaguzi wa rangi. Alimuita mchezaji mweusi 'nyani' na akashtakiwa kwa kosa hilo na kukutwa na hatia - akapewa adhabu ya kulipa faini na kusimamishwa mechi kadhaa.

Kiungo wa kati: Joey Barton - QPR. 

Inawezekana ndio mchezaji ambaye ametuhumiwa kwa makosa mengi kuliko wote kwenye kikosi hiki.  Kuendesha gari kwa kasi kubwa, Kupigana, Kuendesha huku amelewa, kupigana na mapolisi na listi inaendelea zaidi. Mwaka huu alijaribu hata kuwatukana Neymar na Thiago Silva kuwaita majina ya ajabu ajabu.Njia pekee ya kumzungumiza huyu ni kumuita kichaa. 

Kiungo wa kati:  Lee Catermole - Sunderland.

 Huyu hafahamiki sana, lakini amekuwa akishikwa sana na mkono wa kisheria. Amekuwa akipigana sana kwenye mabaa na ameshakaa sana rumande, kwa sasa yupo kwenye program iitwayo 'PubWatch' kumuangalia kila anachokifanya akiingia kwenye mabaa.

Winga wa kulia: Jermaine Pennant - Stoke City.

Aliwahi kushtakiwa kwa kutumia madawa ya kulevya, pia amekuwa na sifa ya kupigana kwenye mabaa, aliwahi kufungwa kwa kosa la kuendesha huku amelewa na kusababisha ajali. Amewahi kuvitumikia vikosi vya Arsenal na Liverpool.

Winga wa kushoto: Frank Riberry - Bayern Munich.

Winga huyu wa Bayern Munich anatuhumiwa na kesi ya ubakaji kwa kufanya mapenzi na changudoa ambaye ana umri mdogo. Alikuwa kwenye timu ya taifa ya Ufaransa na akaagiza aitiwe changudoa chumbani kwake ndipo alipokutana na binti huyo mdogo. 

Mshambuliaji: Luis Suarez - Liverpool

Hapa nilipata mtihani kidogo kuchagua kati ya Suarez au Balotelli, lakini mshambuliaji huyu wa Liverpool ameweza kushinda kuchukua jukumu la mshambuliaji wa kati. Ameshakutwa na hatia katika kesi za ubaguzi, kung'ata wachezaji wenzie, pamoja na kuwapiga. Ni mshambuliaji mkali lakini ana vituko mno.  

Mshambuliaji: Marlon King. 
Aliwahi kukaa jela miezi 18. Alikutwa na hatia kwa kumpiga kichwa mchezaji mwenzie Dean Windass wakiwa casino. Aliiba gari la BMW. Kwa ujumla ameshawahi kukutwa na hatia ya makosa ya jinai, likiwemo la kumpiga ngumi ya kichwa msichana wake, kuendesha kwa kasi huku akiwa amelewa. 

Huyu anastahili nafasi mbele ya Lionel Messi mwenye kesi ya kukwepa kodi, na mtukutu Balotelli.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...