Shabiki wa Manchester United Bwana Peter Bolton inawezekana ndiye mshabiki namba moja wa timu hiyo.
Bolton
mwenye miaka 56 ambaye anatarajiwa kukwea pipa kuifuata United kwenye
ziara ya pre-season tour barani Asia na Australia, hajawahi kukosa
mchezo hata mmoja wa United ndani ya Old Trafford tangu mwaka 1974 na
Bolton aliwahi hata kuamua kukosa harusi ya kaka kwa ajili ya mechi ya
United.
‘Nilipokutana na mke wangu mwaka 1976 kwenye ukumbi wa disco, aliniuliza kama ningeenda tena wiki ijayo. Nilimjibu “Hapana, nitaenda kuangalia mechi dhidi ya Spurs White Hart Lane, tangu siku hiyo aligundua maisha yangu yanazungukwa na soka. Mwaka 1979, tulikuwa tumepanga kufunga ndoa na ilibidi nichague mwezi wa sita - kwa sababu nilijua hakuna soka mwezi huo!’
‘Wakati
kaka yangu alipokuwa anaoa, alipanga tarehe ambayo iliangukia wikiendi
katikati ya msimu. Nilibaki njia panda kwa sababu kulikuwa kuna mechi ya
United ikicheza.... baadae niliamua kwenda kuangalia mechi Old Trafford
na usiku nikaenda kwenye party ya harusi. Kaka yangu hakukasirika,
alifahamu namna ninavyopenda kuiona United ikicheza.’
Wiki hii, Bolton anakwea pipa kwenda Sydney kwa ajili ya kuiangalia timu yake aipendayo ikijiandaa na msimu mpya - hakuenda Bangkok lakini sasa atakuwa na wiki tatu zenye mihangaiko kuliko akisafiri maili 30,000 na kutumia masaa zaidi ya 50 hewani kuifuata timu ya David Moyes kwenye pre season.
Bolton,
ambaye anaishi maili kadhaa kutoka Old Trafford huko Timperley,
anasema: ‘Nina mashaka kama nitabakiza chochote katika hizi £5,000 ndani
ya kipindi cha wiki 3 zijazo. Ni vigumu kusema, kwa sababu huwezi
kutabiri matumizi ya fedha lakini sina cha kujutia kwa sababu naenda
kuiangalia timu yangu.
'Nina fahamu namna safari yangu itakavyokuwa, nitasafiri kwa umbali wa maili 30,000 na masaa kama 55 hewani. Tatizo ni kwamba hakuna hata ndege moja itakayokuwa ikienda moja kwa moja.
Gary Neville akisimama na bendera ya bwana Bolton yenye maandishi ya 'One Love'
‘Nitatoka
Manchester mpaka Sydney kupitia Dubai. Then Sydney mpaka Yokohama
kupitia South Korea. Halafu nitachukua treni mpaka Osaka kabla ya
kuelekea Hong Kong kupitia Shanghai. Halafu nitakuwa narudi nyumbani
Manchester kupitia Dubai na baada ya hapo safari itakuwa inaelekea
Stockholm Sweden. Lakini hata kutokea kurudi nyumbani itabidi nipitie
Oslo!'
Bolton,
ambaye ameshahudhuria mechi za United za nyumbani zaidi ya 1,000
mfululizo na amekuwa akishabikiwa United tangu mwaka 1962, pia amekuwa
akifuatilia mechi za timu ya vijana ya United pale Old Trafford.
‘Niliangalia
michezo 120 katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita. Ikiwa timu ya
wakubwa haichezi, najaribu kufuatila timu ya vijana na timu ya reserve
pia nyumbani na ugenini. Mwaka uliopita nilienda kuangalia wakicheza na
Swansea na Southampton ugenini nikiisapoti timu ya vijana.
‘Mke
wangu anajua ninavyopenda soka na kuna siku nyingi ndani ya mwaka
ambazo ninatumia kuwa nae na familia kiujumla. Kwangu mimi soka ni kama
kilevi changu, kwangu mimi ni familia na soka ndio vitu muhimu.'
Bolton
na bendera yake ya akiishangilia United. Amesema kwamba mashabiki wa
Atletico Bilbao ndio wastaarabu kuliko wote ambao amewahi kukutana nao.
No comments:
Post a Comment