Taarifa zinaeleza kuwa Simba ambayo ndiyo ilikuwa ya kwanza kumuwania mchezaji huyo, inakamilisha mipango ya kumsajili na ndiyo ambayo imepanga kumleta nchini siku hiyo, lakini Yanga nayo inamhitaji na tayari ilishatuma mtu Vietnam.
Inaelezwa kuwa wakati Simba ikikamilisha mpango huo wa kumleta nchini Agosti 28, tayari Yanga nayo imeanza mipango ya kuwapiga bao wapinzani wao hao, kama ilivyofanya kwa Mbuyu Twite, msimu uliopita.
Chanzo makini cha habari kutoka Simba kimesema kiungo huyo aliyebakiza mkataba wa miezi miwili nchini Vietnam, anasubiri ligi kuu ya nchini humo imalizike kabla ya kutua Msimbazi.
Chanzo hicho kilisema klabu hiyo itafanya jitihada zote ili isimkose kiungo huyo raia wa Uganda, kwani haitaki kushuhudia akitua kwa wapinzani wao hao wa jadi, Yanga.
“Mara baada tu ya mchezaji huyo kuwasili, tutaanza kushughulikia ITC (Hati ya Uhamisho wa Kimataifa) yake ili tuweze kummiliki rasmi,” kilisema chanzo hicho na kuendelea:
“Ligi yao ya Vietnam inamalizika Agosti 27, kisha siku moja baadaye ataondoka kuja huku, tayari ameshaomba release (ruhusa) kwenye klabu yake ili aje nchini kwa ajili ya kukamilisha usajili wake.
“Unajua Yanga wamekuwa wakituingilia katika masuala yetu ya usajili, hivyo tunafanya hivyo ili kukamilisha dili mapema.”
Licha ya kuwepo na taarifa za kukanusha juu ya Yanga kufanya mazungumzo na mchezaji huyo, Championi lina uhakika kuwa kigogo wa Yanga alitua nchini Vietnam wiki ya juzi na kuzungumza naye lakini hawakufikia muafaka, hivyo atakapotua hapa nchini siku hiyo, ndiyo kila kitu kitakuwa wazi.
No comments:
Post a Comment