Mwanamke mmoja Sumayi Girandi mkazi wa kijiji cha Kunzugu wilayani Bunda amepoteza vidole vitatu vya mkono wa kulia na kiganja cha mkono wa kushoto kukatwa baada kushambuliwa kwa mapanga na watu wasiojulikana kisa kikidaiwa kuwa kutaka kunyang’anywa mali zake.
Uhodari
wa mama huyo wa kutafuta mafanikio ya familia yake hasa baada ya
kutengana na mume wake umeishia hapo baada ya watu wasiojulikana
kumvamia nyumbani kwake na kumshambulia kwa mapanga na kisha
wakamkata kiganja cha mkono wa kushoto na kuanguka.
Kwa
sasa Sumayi Girandi anatibiwa katika Hospitali teule ya wilaya.
Vitendo vya kujeruhi na kuua wanawake mkoani Mara kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo ya ndugu kutaka kuwanyang’anya bado vinaendelea.
Katika
tukio lingine wilayani Bunda dereva mmoja wa pikipiki ameuawa na watu
wasiojulikana ambapo taarifa zinasema kuwa kabla ya kuuawa kwa dereva
huyo wa bodaboda inadaiwa alikodiwa na watu wawili.
Kamanda
wa Polisi wa mkoa wa Mara Ferdinand Mtui amethibitisha kutokea kwa
matukio hayo na tayari watu wanne wamekamatwa wakiwemo watu
wanaotuhumiwa kumkatakata mapanga mwanamke Sumayi Girandi.
Emmanuel Amas, TBC Mara.
No comments:
Post a Comment