facebook likes

Tuesday, July 9, 2013

GENEVIEVE AKABIDHI JUMBA KWA WAZAZI WAKE



ZAENI matunda mema! Ndivyo wanavyoweza kusema wazazi wa mwigizaji maarufu nchini  Genevieve Nnaji baada ya kukabidhiwa nyumba ya kifahari na mtoto wao.

Mioyo ya wazazi hayo iko poa baada ya mwanadada huyo mwenye mvuto kuwahamishia katika jumba la kifahari lililopo eneo la watu maarufu jijini Lagos. Eneo hilo linajulikana kama Lekki.


Awali familia hiyo ilikuwa ikiishi eneo la Egbeda, ambako huishi watu wa kariba ya kawaida. Mama wa msanii huyo ameshagota umri wa miaka 60 na mshua ana miaka 70.


Kwa mujibu wa watu walio karibu na familia hiyo, ilikuwa furaha ya aina yake kwa wazee hao kupata makao mapya yenye hadhi inayostahili.


Genevieve, ameamua kutoa nyumba hiyo kwa wazazi kama sehemu tu ya shukrani. Lakini pia kuwahamishia eneo hilo kutarahisisha upatikanaji wa huduma za msingi kama vile matibabu.Imeripotiwa kuwa baba yake anashindwa kutembea umbali mrefu kwa sababu ana matatizo ya miguu.



Awali wazazi hao walikuwa katika mazingira yasiyoridhisha pamoja na ukweli kwamba binti yao ana uwezo wa kuwatunza.Lakini ukweli wa mambo ni kwamba hii si mara ya kwanza kwa binti huyo kuwakumbuka wazazi wake. Kila kipato chake kinapoongezeka, amekuwa na tabia ya kuboresha mazingira ya familia yake.


Majirani wanasema wazazi wa msanii huyo ni watulivu na wachamungu na kwamba huwezi amini kuwa binti yao ni staa anayekubalika katika mengi ndani na nje ya Afrika

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...