Baada ya kuondokewa na kipenzi chake cha karibu (Ngwea), M2thep amesema
yuko mbioni kuchora tattoo kubwa yenye sura ya Ngwea mgongoni katika
kumkumbuka kwake, na kwasababu alipokuwa nae South Africa mara ya mwisho
alimtakia kuwa anataka kuchora tattoo.
"Tattoo ya chozi hii niliichora kwasababu ya kuondokewa na mama yangu
mzazi, hii inaashiria nilipoondokewa na mama yangu, then niliweza
kuchora tattoo hii ya chozi, yaah nikachora tattoo hii ya chozi,
nikachora tattoo ya music mkononi, ambapo mi ni blood ambae napenda sana
music, nikachora melody kwenye shingo,then nataka kuchora tattoo kubwa
ngongoni yenye picha yake, nadhani itakuwa ndio kumbukumbu yangu kubwa,
ambayo ntaichora mgongoni, kichwa kizima cha Albert nitakichora, yaani
nategemea hicho kitu kukifanya, yaani ntakapo tulia nadhani,
ntakapotulia ntaweza kufanya hicho kitu, kwasababu sasa hivi yenyewe
ndio nimeanza ku recover, na natoka toka sasa hivi na vitu vingi
vinanihusu studio nini, ila nikipata muda ndio ambacho cha muhimu, yaani
hata yeye mwenyewe kwanza kipindi anakuja soth africa alisema mwenyewe
anataka kuchora tatto, lakini kwa bahati mbaya mpaka anaondoka hajaweza
kuchora hiyo tatto ambayo alikuwa anaitarajia yeye wenyewe kuichora,
ambacho mi ndio nitakachokifanya kumuenzi, ntachora tattoo kubwa
mgongoni ambayo itakuwa na picha yake" amesema M2thep.
No comments:
Post a Comment